Shida za kifedha zinamkaba Tombi, na anaanza kupanga na rafiki yake namna ya kupata pesa zaidi . Lakini wakati mipango yao ikiendelea, mambo yanachukua sura mpya upande wa kina Hambe… Tunaona wake wengine wakikusanyika, huku Shupiwe akisimulia kwa kujivunia jinsi alivyomkabili na “kummaliza” mchawi kwa kutumia maji ya upako. Simulizi hilo linatikisa kila mtu — mashaka na hofu vikianza kutanda juu ya kile kilichotokea kweli. Mpali inaendelea kutuonyesha kuwa tamaa, imani na hofu zikichanganyika — matokeo yake huwa mazito kuliko tunavyodhani…