Kibibi na Roy wanaanza ukurasa mpya kwa kufanya kazi pamoja kwenye club . Lakini mambo hayaendi kama alivyotarajia, kwani Roy anaonekana kulewa kazini—jambo linalomkasirisha sana Kibibi. Katika hasira na maumivu, Kibibi anamwambia wazi kuwa hana msaada wowote… na penzi lao linaanza kuyumba . Wakati huo huo, tunamuona Tajiri akimshauri Ritha kwa busara: ugomvi haujengi, ni muhimu kutafuta njia za hekima kupata suluhu . Lakini je, ushauri huo utasikilizwa? Au moto wa migogoro utaendelea kuwaka