Mpungwe anaangukia pabaya baada ya polisi kufika nyumbani kwake na kumkamata . Ni Fahad anayeongozana nao — akiamini huu ndio wakati wa Mpungwe kujibu maswali yake yote. Lakini mambo yanabadilika ghafla pale anapokutana uso kwa uso na Sikujua… na maneno ya kejeli yanarushwa bila huruma. Mvutano unazidi kupanda — huku hofu ikitanda juu ya hatma ya Mpungwe. JIVU linaendelea kutuonyesha kuwa kila siri ina mwisho — na wakati haki inapogonga hodi, hakuna wa kuizuia…