Bobo (Van Vicker) alionekana kwenye vipindi vichache mwanzoni wa msimuu huu wa Jua Kali baada ya kusafiri kutoka Ghana mpaka Tanzania kukutana na mpenzi wake wa zamani, Anna. Alivyokuwa Tanzania, mambo hayakuenda vizuri na kwa bahati mbaya aliondoka na moyo wake ukiwa umevunjika.
Anna alivyofika Ghana alikutana na rafiki yake toka chuoni, Linda, na Linda aamua kumpeleka kwa Bobo. Baada ya Bobo kurudi Ghana toka Tanzania, moyo wake ulikuwa mgumu, na alimwambia shangazi yake, Auntie Zozo (Patience Ozokwor) kuhusu yote aliyomkuta alivyokuwa Tanzania. Aunty Bobo bado ana hasira na Anna na akataa kabisa kuwapokea Anna na Linda. Kwa sasa hivi, Anna amekwama na jinsi ya kuonana na Bobo tena. Je atafanikiwa kumuona Bobo kwenye safari hii?
Usikose kuangalia #MMBJuaKali kila Jumatano hadi Ijumaa saa 3:3o usiku ndani ya DSTV chaneli 160!