Ikiwa ni zaidi ya miongo miwili akiwa katika tasnia ya uigizaji, Patience Ozokwor amejitwalia umaarufu mkubwa katika tasnia ya filamu na burudani. Ukitazama neno "kipaji" katika kamusi, bila shaka utapata jina la Patience na vilevile majukumu ya kipekee ambayo amecheza katika maisha yake yote ya uigizaji.
Mshindi wa tuzo na mwigizaji nguli (anayejulikana kwa jina la Mama G) sasa ataonekana kwa mara ya kwanza katika tamthilia ya Jua Kali mnamo Jumatano 16 Machi kama shangazi wa Zozo- Bobo. "Tunafuraha na ni heshima kubwa kufanya kazi pamoja na Patience Ozokwor na tunatarajia mapinduzi makubwa katika tamthilia ya Jua Kali," alisema Barbara Kambogi, Mkuu wa Chaneli ya Maisha Magic Bongo.
Kutana na Patience kwenye #MMBJuaKali kuanzia tarehe 16 Machi na kila Jumatano hadi Ijumaa saa 9.30 usiku .Kutokana na maombi ya watazamaji na wapenzi wa tamthilia ya #MMBJuaKali, tamthilia hii itakua ikirushwa mara tano kwa wiki kila Jumatano hadi Jumapili kuanzia tarehe 30 Machi. Ndiyo, maoni yametufikia na tumeyafanyia kazi, usikose kutazama yanayojiri katika tamthilia ya #MMBJuaKali.