Logo
channel logo dark

Jua Kali

160Tamthilia16

Je Mr Smile ndiye wa milele kwa Anna? - Jua Kali

Habari
24 Novemba 2021
Mr Smile atua Tanzania na yupo tayari kumuona Anna.
Screenshot 2021 11 24 at 15

Anna ana imani kubwa juu ya mapenzi ila bahati alikuwa hana. Tangu mwanzo alipenda sana kuanzia na George, ambaye alimpenda san na kudhani kwamba atakuwa nae milele. Lakini siku ambayo alikuwa akutane nae uwanja wa ndege na waanze maisha pamoja, aligundua kwamba George alikuwa na mke na mtoto na pia mke wake alikuwa ni mjamzito.  Baada ya George akaja, Dominic, kijana wa mjini, na Dominic aliamua kumuacha siku ya harusi. Lakini Anna hakufa moyo na baadae alikutana na Dr Temba, Dr Temba na Anna walipendana sana lakini Mungu alimpenda Dr Temba zaidi. Kwenye siku yao ya harusi, Dr Temba alipata ajali na kufariki.

Baada ya hizo taabu zote, Anna alijihisi kwamba hana bahati na mapenzi. Kifo cha Dr Temba kilimfanya karibu awe kichaa. Baada ya kuomboleza kwa muda mwingi, familia yake na marafiki zake waliona kwamba tabasamu ilianza kurudi kidogo kwa Anna.

Iligundulika kwamba Anna alirudisha mawasiliano na rafiki yake wa zamani aliyesoma nae, Mr Smile. Mr Smile na Anna walipenda ingawa Mr Smile alikuwa nje ya nchi. Baada ya muda, Mr Smile aliamua kuja Tanzania juu ya Anna.

Je unafikiri, Anna atapata bahati na mapenzi sasa? Fuatilia #MMBJuaKali kila Jumatano hadi Ijumaa saa 3:30 ndani ya Maisha Magic Bongo, Chaneli 160!

Screenshot 2021 11 24 at 15
Je Mr Smile ndiye wa milele kwa Anna? - Jua Kali

Je unafikiri, Anna atapata bahati na mapenzi sasa?

Ndiyo79%
Hapana21%