Mpango uliopangwa kwa ujanja unaanza kuvunjika. Maya anampigia Enzo simu bila kutarajiwa, jambo linalomkasirisha na kuzua taharuki kubwa. Walikubaliana kuigiza kama wapo kwenye mahusiano ya uongo ili kumzuga Patrick, asigundue kuwa mkewe Regina yuko kwenye uhusiano wa siri na Enzo.Lakini kadri muda unavyosonga, mipango inachanganyikiwa. Hisia za kweli zinaanza kuibuka kati ya Maya na Enzo, zikivunja mipaka ya makubaliano yao. Wakati huo huo, uhusiano wa Regina na Enzo unaendelea kuwa tishio kubwa. Je, ukweli ukifichuka, nani ataumia zaidi?