Mambo yanazidi kuwa mazito ndani ya Huba huku uhusiano wa Tajiri na Nicole ukitingishwa na migongano, mashaka na maamuzi yanayoumiza. Kila hatua wanayochukua inaibua maswali mapya — je, mapenzi yao yana nguvu ya kustahimili presha hii, au ukweli unaokuja utavunja kila kitu?Wakati hisia zikizidi kupanda, pande zinazowazunguka zinaanza kuathiri hatima yao, na kufanya hali kuwa ngumu zaidi kuliko walivyotarajia. Hatima ya Tajiri na Nicole bado ni kitendawili.