Logo
channel logo dark

Kumi Za Wiki

160Muziki13

Malkia wa Bongo Flava ndani ya #MMBKumiZaWiki

Habari
03 Machi 2022
Ni mwezi wa wanawake na tunasherekea wasanii wetu wa kike wanaovuma ndani ya kipindi cha Kumi za Wiki!
Untitled design (10)

Mwezi wa tatu ni mwezi wa wanawake kimataifa, tarehe 8 Mwezi wa tatu ni sikukuu ya wanawake kimataifa. Kusherekea hii siku kuweka orodha ya baadhi ya wanamuziki wa Bongo Flava wa kike wanaovuma kwenye kipindi cha #MMBKumiZaWiki.

Nandy

Nandy AKA ‘The African Princess’ ni mwanamziki bingwa ndani ya bara la Afrika. Pamoja na muziki wake, ni muigizaji mzuri pia ambaye unaweza kumuona ndani ya kipindi cha #MMBHuba kila Jumatatu hadi Ijumaa saa 3 usiku ndani ya Maisha Magic Bongo. Kwa sasa unaweza pia kusiliza nyimbo yake na Bilnass na Mr Eazi, inayoitwa ‘Party’ ikiwa inavuma kwenye chati ya #MMBKumiZaWiki.

Genevieve

Genevieve au Phina ndani ya kipindi cha #MMBSinia kila Jumamosi na Jumapili saa 3 usiku, Phin ani mke wa Cosmas. Kwenye muziki pia yumo na unaweza kuuangalia mwimbo wake unaoitwa ‘Moto’ ndani ya #MMBKumiZaWiki

Zuchu

Umaarufu wa Zuchu unazidi kuvuma nchini Tanzania, je unajua kwamba Zuchu ni ndugu yake na Bi. Khadijah Kopa mwuimbaji maarufu wa Taarab una mama yake Michael ndani ya kipindi cha #MMBJuaKali kila Jumatano hadi Ijumaa saa 3:30 usiku ndani ya Maisha Magic Bongo. Usikose kuangalia nyimbo ya Zuchu inayovuma ndani #MMBKumiZaWiki inayoitwa, ‘Mwambieni’.

Rosa Ree

Unaweza kumtamtambua Rosa Ree toka ndani ya kipindi cha #MMBSinia, alivyoigiza kama Leila. Pia ukiacho hivyo, hivi karibuni alionekana ndani ya kipindi cha DStv kinachovuma duniani kinachoitwa ’90 Day Fiance’. Usikose kuangalia nyimbo yake inayoitwa, “Mulla” pamoja na Abby Chams ndani ya #MMBKumiZaWiki.

Kati ya hizi nyimbo, ni wimbo gani umependelea zaidi?👇👇

Wimbo unauopenda zaidi! - Kumi Za Wiki

Kati ya hizi nyimbo, ni wimbo gani umependelea zaidi? Chagua hapo chini

Nandy ft. Bilnass & Mr Eazi - Party17%
Geneveive - Moto13%
Zuchu - Mwambieni61%
Rosa Ree ft. Abby Chams - Mulla9%

Kumbuka kuburudika na #MMBKumiZaWiki kila Ijumaa saa 11 jioni ndani ya Maisha Magic Bongo!