Logo
Divas & Hustlas
channel logo dark

Divas And Hustlas

160Lifestyle16

Pata kujua nani ni nani ndani ya kipindi kipya kinachovuma Tanzania – Divas & Hustlas

News
11 Julai 2023
Nani ni diva na nani hustla wa Maisha Magic Bongo?
Divas & Hustlas

Kuanzia tarehe 13 Julai tunakuletea kipindi kipya kinachoitwa #MMBDivasAndHustlas kipindi hiki kitafuatilia wanaburudani wanaongoza Tanzania. Pata kujua nani ni nani hapo chini:

MALKIA KAREN

Karen ni malkia wa ulimwengu wake. Baada ya mapumziko mafupi ndani ya kazi yake ya muziki, Malkia Karen ana hamu ya kurudi kwenye muziki. Dada huyu ni mfanyabiashara na yupo tayari kufanya kazi ya kujenga jina lake ndani ya sekta ya muziki nchini, na pia yeye ni mjasiriamali wa baa maarufu ya juisi.

ZEE CUTY

Zee ndiyo picha kamili pekee, muonekano wake ndiyo kitu muhimu sana kwake na anahakikisha popote alipo anakuwa akipendeza. Zee yuko tayari kupanua kipaji chake cha kutengeneza nywele na kama mwanamitindo katika tasnia hii. Kimuziki ametoa nyimbo zake na yupo tayari kujulikana kama mwimbaji bora.

 

KONTAWA

Kwa umaarufu anajulikana kama Tawa, na alitoa nyimbo zake chini ya hilo jina. Yeye ni nyota mkubwa na anazidi kupanda. Tawa ni mwanamuziki mwenye kipaji cha kurap pamoja na kuimba, kwa sasa hivi ameingia ndani ya biashara ya mapambo ya nyumbani.

 

CHINO

Chino ni mchezaji ambaye aligeuka kuwa msanii wa kuimba na ana nia ya kuwa mshindani wa juu wa muziki na pia wa biashara. Chino ndiyo kwanza anaanza na muziki, ametoa mtiririko wa nyimbo maarufu na idadi yake ya mashabiki inazidi kukuwa kila siku.

 

KINATA MC

Kitana ni MC na baadhi ya nyota wanaoanzisha utawala kwa kasi ndani ya tasnia hii. Akiwa mwenye furaha na mchangamfu, lakini jambo moja analolichukulia kwa uzito sana ni kazi yake.

 

REYJONES

Reyjones nimuongozaji ndani ya tasnia ya kupanga matamasha na sherehe. Anaheshimika sana kwenye tasnia hii kwa kuwa mtu asiyependa upuuzi na kuwa mchapakazi. Pia anafanya kazi kama mpangaji wa matamasha makubwa ya wanamuziki wanaongoza nchini na pia anaaminika na shughuli za kiserikali. Reyjones anafanya yote wakati akiwa mume na baba wa watoto wawili.

 

Usikose kipindi cha #MMBDivasAndHustlas kila Alhamisi saa 1 usiku ndani ya DStv chaneli 160!

Divas & Hustlas
Divas & Hustlas - Maisha Magic Bongo

Je uliangalia kipindi cha kwanza cha #MMBDivasAndHustlas?

Ndiyo, sikuweza kukosa!!75%
Hapana, nitaangalia marudio!25%