Logo
Wana wa Town

Mapinduzi ya burudani na vipindi vipya ndani ya Maisha Magic Bongo!

Habari
24 Januari 2024
#MMBWanaWaTown kuanza tarehe 4 Februari na #MMBNuru kuanza tarehe 5 Februari
Article

Tunaanza mwezi ujawo wa Februari na vipindi viwili vipya. Kuanzia Jumapili, tarehe 4 Februari, saa 4 usiku, tunakuletea kipindi cha #MMBWanaWaTown pia tukifuatilia na kipindi cha #MMBNuru kuanza Jumatatu, tarehe 5 Februari, saa 4 usiku.

WANA WA TOWN

Kipindi hiki kina wafuatilia vijana wanne (Whozu, Calisah, Brown na Country Boy) wenye ushawishi, umaarufu, pesa na utanashati kwa mara ya kwanza wanatuonyesha maisha yao halisi, panda shuka zao za kazi, mapenzi, familia na mengine chungu nzima. Jiunge nasi kuanzia Jumapili, tarehe 4 saa 4 usiku na kila Jumapili ifuatayo.

Angalia video ya mwanzo wa #MMBWanaWaTown

 

NURU

Kuanzia Jumatatu tarehe 5 Februari tunakuletea tamthilia mpya ya inayoitwa Nuru, tamthilia hii inahusu ndugu wawili waliochukiana wanajikuta lazima waungane kupambana na adui anaewatandia giza nene maishani mwao, baba yao. Usikose tamthilia hii kuanzia tarehe 5 Februari na kila Jumatatu hadi Ijumaa saa 4 usiku ndani ya #MaishaMagicBongo.

Angalia video ya mwanzo wa #MMBNuru

 

Endelea kufuatilia vipindi hivi ndani ya Maisha Magic Bongo kupitia DStv chaneli 160!