Logo
Wana wa Town

Mabachela wa Wana wa Town

Habari
19 Machi 2024
Juana na wana wa town wanaoowasha moto television zetu kila Jumapili saa 4 usiku!
Wana wa Town

Wana wa Town ni kipindi kipya ndani ya DStv Maisha Magic Bongo. Kipindi hiki kinafuatilia mabachela wanne

WHOZU

Whozu ni msanii mkali wa muziki wa Bongo flava na siku zote yeye ni mpenda burudani na pia ni Maisha ya pati yoyote. Ukiachana na muziki, Whozu pia yupo ndani ya mahusiano na staa mkubwa na Tanzanian Sweetheart, Wema Sepetu. Pamoja na hayo, pia ni mdogo wake mwanamitindo maarufu Frank K.

 

CALISAH

Calisah ni mwanamitindo maarufu anayejulikana kwa Maisha yake ya kifahari na kuchumba wanawake wengi maarufu kataika tasnia ya burudani nchini Tanzania. Yeye ni zaidi ya muonekano wake tuu, ni mtu anayependa kupiga mahesabu ya kali na anapenda kupata njia yake kwenye kila kitu.

BROWN

Brown pia ni mwanamitindo anayejulikana kwa uzungumzaji wake wa wazi na kupenda sana na madada. Anajoina kama yeye ndiye kilele cha juu ndani ya ulimwengu wa wanamitindo na hamna chochote kitakacho mkosesha nafasi ya juu.

 

COUNTRY BOY

Country Boy ni mwanamuziki wa rap, alitiwa moyo na kaka yake mkubwa, kikongwe wa redio, Babuu wa Kitaa. Kwa sasa, Country Boy amejezeka kama mwandishi mkubwa wa muziki wa rap na MC bora ingawa muda wake kwenye tasnia ya muziki, na kwa sasa amesaini na genge la Konde la muziku chini ya msanii Harmonize.

Mabachela wa #MMBWanaWaTown

Kati ya hawa ni nani umemkubali zaidi?

Click here to make your selection
Wana wa Town
Whozu
Wana wa Town
Calisah
Wana wa Town
Brown
Wana wa Town
Country Boy

 

Jiunge nasi kila Jumapili saa 4 usiku kwa vipindi vipya vya #MMBWanaWaTown