channel logo dark
kapuni
channel logo dark

Kapuni

160DramaPG13

Samabaza jina

Uchungu wa mapenzi – Kapuni

00:04:43
Robert anaenda sambamba na Brown , Ofisini Moto Jordan, Paul na Joyce mambo hayaeleweki Koku bado ana mganda Jordan, mtaani vituko kwenda mbele.John amegoma kazi.
Uchungu wa mapenzi – Kapuni Image : 1068

Vipindi Zaidi

Tamthilia Zetu on Maisha Magic Bongo

Razia Azidiwa, Balui Akata Tamaa – JIVU Image : 2292
Mwanida Achoshwa na Tabia za Frank – Mpali Image : 2293
Mwanida Achoshwa na Tabia za Frank – MpaliMwanida anamwambia wazi Frank kuwa amechoshwa kuhusishwa na matukio yake ya kihalifu. Wakati huohuo, Hambe na mkewe wanabaki kuchanganyikiwa baada ya kugundua kwamba polisi wameanza kufahamu michezo yao ya kificho.
Kibibi Aachiwa, Kesi Yafutwa – Huba Image : 2291
Kibibi Aachiwa, Kesi Yafutwa – HubaKibibi anashangaa pale anapoambiwa kesi yake imefutwa na wakubwa bila kueleza zaidi nani alikuwa mshitaki. Wakati huo, Ritha na Nicole wanakutana uso kwa uso kwenye mzozo mkali unaoleta msuguano mpya. Lakini mambo yanachukua mwelekeo tofauti pale Kibibi anapokutana na Ray na Faudhia—akiwa na furaha na matumaini mapya ya kufanya biashara na Ray.
Mitihani ya Bilu inazidi kuwa mizito kwenye JIVU! Image : 2287
Mitihani ya Bilu inazidi kuwa mizito kwenye JIVU!Safari hii, maskini Bilu amesingiziwa wizi na raia wenye hasira wakamgeuzia kisasi bila huruma. Je, ataweza kujinasua na kutafuta haki, au hili litazidi kumuangusha zaidi?
Vita ya Kamishna na Zulu Brothers – The Wife Image : 2288
Vita ya Kamishna na Zulu Brothers – The WifeKisasi cha Kamishna kimefika hatua ya hatari! Akiwa bado na majonzi ya kifo cha mkewe, anawageukia Zulu Brothers na kuanzisha vita kali dhidi yao. Lakini je, Zulu Brothers watasalimu amri au vita hii itageuka kuwa damu juu ya damu?
Zulu Brothers Wakamatwa na Kamishna – The Wife Image : 2273
Zulu Brothers Wakamatwa na Kamishna – The WifeMambo yanazidi kushika moto kwenye The Wife! Kamishna anawakamata Zulu Brothers na safari yao inaishia sero . Lakini kubwa zaidi—Mahlomu akutwa na ujauzito! Je, ni wa mume wake Mqhele au wa Qhawe, kaka yake?
Mpango wa Ndoa Wafeli – JIVU Image : 2270
Mpango wa Ndoa Wafeli – JIVUFamilia ya Bi Barke wanakiri kuwa mpango wao wa kumlazimisha Fahad kumuoa Sada umefeli kabisa . Wanalazimika kuukubali ukweli na kumrudisha Fahad kwao. Lakini mambo yanageuka kuwa mazito zaidi pale Ajuaje anaanguka na kuzimia.
Frank Ahisi Mtoto Si Wake – Mpali Image : 2272
Frank Ahisi Mtoto Si Wake – MpaliMwanida anajikuta kwenye hali ngumu baada ya Frank kuanza kuhisi mtoto si wake . Wasiwasi huu unaweza kutikisa ndoa na familia yao nzima. Wakati huo huo, Lindiwe anaingia kwenye malumbano makali na binti yake Bupe kuhusu pombe . Lakini majibu ya Bupe yanatikisa zaidi — anasema chanzo cha ulevi ni mama yake mwenyewe! Familia ya Nguzu inazidi kuyumba huku kila siri ikileta maumivu mapya.
Bill Amvisha Eva Pete ya Uchumba Image : 2271
Bill Amvisha Eva Pete ya UchumbaMapenzi ya Bill na Eva yamezidi kupamba moto! Hatimaye Bill anathibitisha hisia zake kwa kumvisha Eva pete ya uchumba, na sasa harusi inanukia.
Tima na Ray nyumbani kwa Ritha – Huba Image : 2269
Tima na Ray nyumbani kwa Ritha – HubaRay na Tima wanajikuta wamekutana kwa Ritha , wanabaki na mshangao. Lakini tension inaongezeka zaidi pale Tima anapompeleka Chidy hospitali kwa ajili ya matibabu ya afya ya akili . Wakati huo, Kibibi na Roy wakiendelea na mapambano juu ya umiliki wa nyumba.
Wanajoola Wamwambia Kamishna Zulu Brothers Wamemuua Mke Wake Image : 2263
Wanajoola Wamwambia Kamishna Zulu Brothers Wamemuua Mke WakeMambo yanazidi kuwa ya kusisimua! Wanajoola wanamwambia Kamishna kwamba Zulu Brothers wamemuua mke wake, na taarifa hii inasababisha msukosuko mkubwa ndani ya jamii. Wakati huo huo, Zandile anafunguliwa mlango mpya wa maisha baada ya kutoka jela pale anakutana na mtoto wake. Lakini mtoto anakuwa mgumu kumkubali, akidai kuwa walimwambia mama yake amekufa. Je, Zandile ataweza kushinda changamoto hii na kujenga upya uhusiano na mtoto wake?
Mchuma na Mpungwe Wakimvamia Fahad – Fahad Awaonya Kina Sikujua I JIVU Image : 2266
Mchuma na Mpungwe Wakimvamia Fahad – Fahad Awaonya Kina Sikujua I JIVUMambo yanazidi kuwa ya kusisimua! Mchuma na Mpungwe wanamvamia Fahad kwa ghafla, wakimshambulia bila kuwa tayari. Hali inazidi kuwa ya hatari pale Fahad anapoamua kwenda kwa Kina Sikujua kumwonya kuhusu mkewe, ambaye hajajua kuhusu mimba aliyokuwa nayo. Je, hatua hii ya Fahad itasaidia kulinda familia yake au kuanza mfululizo wa matatizo mapya? Tukufueni kuona jinsi uhusiano na siri zinavyoibuka katika JIVU.
Shupiwe Akidai Hela Zake – Mwanida Aondoka Nyumbani I Mpali I S6 I Ep 28–31 I Maisha Magic Bongo Image : 2264
Shupiwe Akidai Hela Zake – Mwanida Aondoka Nyumbani I Mpali I S6 I Ep 28–31 I Maisha Magic BongoShupiwe anachukua hatua ya kudai hela zake za Bar, lakini hali inakuwa ngumu zaidi kwa Mwanida na Frank. Mwanida ameondoka nyumbani, akimwacha Frank pamoja na mtoto wake. Je, uamuzi huu utaleta utulivu au kuanza kwa changamoto mpya?
Ray na Abby Wakimbia Nyumbani – Huba I S14 I Ep 75–77 I Maisha Magic Bongo Image : 2262
Ray na Abby Wakimbia Nyumbani – Huba I S14 I Ep 75–77 I Maisha Magic BongoRay na Abby wanachukua uamuzi mgumu — kuikimbia nyumba! Lakini je, kukimbia kutawapatia suluhisho au ni mwanzo wa maafa mapya? Mambo yanageuka hatari zaidi pale Ray anapomvamia Tima na kumshikia bastola . Tima anakutana uso kwa uso na hofu, huku kila mtu akijiuliza — je, Ray amefikia wapi? Je, hatua hii ya Ray itabadilisha hatima ya wote walioko karibu naye?
Mqhele Amuua Sandile – Mapenzi ya Hlomu Yageuka Damu I The Wife I S1 I Ep 39-40 I Maisha Magic Bongo Image : 2261
Mqhele Amuua Sandile – Mapenzi ya Hlomu Yageuka Damu I The Wife I S1 I Ep 39-40 I Maisha Magic BongoHasira za Mqhele zinampeleka mbali — anamnyang’anya uhai Sandile baada ya kugundua uhusiano wake na Hlomu. Wakati Hlomu akienda kumtembelea Sandile, anakutana na hali ya kutisha: Sandile tayari ameuwawa! Wakati huo huo, ndugu wa Zulu Brothers wanafanikisha mpango wao wa kumtorosha Zandile gerezani, hali inayoongeza moto kwenye drama hii ya kifamilia na kimapenzi.
Fahad Akiri Kutokuwa Tayari Kuwa Baba – JIVU I S1 I Ep 39-40 I Maisha Magic Bongo Image : 2260
Fahad Akiri Kutokuwa Tayari Kuwa Baba – JIVU I S1 I Ep 39-40 I Maisha Magic BongoFahad anamueleza mkewe Razia kuhusu mimba, akionekana wazi hayuko tayari kubeba majukumu ya baba . Anakiri mimba hiyo inamchanganya sana, lakini Razia anaendelea kumsihi waiachie akazalie mtoto huyo. (Lakini kumbuka — mimba hiyo ni ya Kawia! ) Wakati huo huo, Ajuaje anamkabili binti yake Sikujua baada ya kugundua mimba aliyobeba baba yake ni Fahad. Majibizano makali ya mama na mtoto yanatibua hali, siri zikifichuka na maumivu kuongezeka. Je, ukweli huu utazidi kuivunja familia hii?
Mwanida Aingiwa na Wasiwasi kwa Frank – Mpali I S6 I Ep 25-28 I Maisha Magic Bongo Image : 2258
Mwanida Aingiwa na Wasiwasi kwa Frank – Mpali I S6 I Ep 25-28 I Maisha Magic BongoMwanida anamfungukia mama yake kuhusu hofu kubwa anayobeba . Anamueleza wazi kuwa Frank amevamia benki, na sasa anaogopa huenda akamvuta naye kwenye hatari hii ya uhalifu! Je, mapenzi ya Mwanida kwa Frank yataendelea kustahimili siri hii nzito, au ni mwanzo wa mwisho wa uhusiano wao?
Malaika na Ray Wakutana Tena – Sura za Zamani Zafichuka I Huba I S14 I Ep 72-74 I Maisha Magic Bongo Image : 2257
Malaika na Ray Wakutana Tena – Sura za Zamani Zafichuka I Huba I S14 I Ep 72-74 I Maisha Magic BongoMalaika na Ray wanaonekana kama wana historia ya zamani. Mazungumzo yao yanamshangaza Malaika, hasa anapomuuliza: “Umetoka tu jela na tayari una mpenzi?” Lakini mambo yanazidi kuwa moto — Abby anamwambia Nelly aachane na Ray, ila Nelly anasimama kidete akimjibu: “Ray amenieleza kila kitu kuhusu wewe — jinsi ulivyokulea na kukukuza.” Je, ukweli huu utavunja uhusiano wa Abby na Nelly, au utafungua ukurasa mpya wa maumivu?
Kifo cha Mke wa Kamishna – The Wife Image : 2251
Kifo cha Mke wa Kamishna – The WifeDrama inazidi kushika moto ! Kamishna anawapa Zulu Brothers jukumu la kumtafuta mke wake – lakini hatarajii kwamba Palesa ameshakufa tayari mikononi mwao. Sasa familia ya Zulu inakabiliana na siri nzito, mtihani mzito na hatari zisizoelezeka, huku kila mmoja akijua kidogo kuhusu ukweli unaowazunguka.
Siri ya Mimba ya Mchuma & Moto wa Mama Karen – JIVU Image : 2250
Siri ya Mimba ya Mchuma & Moto wa Mama Karen – JIVUSikujua anamfungukia Mchuma kuwa mimba aliyobeba ni matokeo ya shinikizo la kulala na Fahad ili Mchuma arejeshwe kazini :scream:. Wakati huo, Mama Karen anaingia kasri la Bi Barke kuibua moto akidai mwanawe aliyenaswa na familia ya Munir kinyume na maridhiano yake.
Kuzo Amfate Mke wa Hambe – Mpali Image : 2252
Kuzo Amfate Mke wa Hambe – MpaliDrama inazidi kunoga ! Kuzo anamuona mke wa Hambe nyumbani na kumtaka amfuate, lakini mke wa Hambe anamwomba aondoke – si sahihi kuwa pale. Wazo ni kwamba wafanye mazungumzo mahali salama zaidi, lakini je, Kuzo ataweza kuzingatia ombi hilo au mapenzi na uhasama yatachukua njia nyingine?
Kofi la Malaika, Vurugu za Tima & Msamaha wa Abby – Huba Image : 2249
Kofi la Malaika, Vurugu za Tima & Msamaha wa Abby – HubaDrama inazidi kupamba moto kwenye #Huba Ray akiwa na Nelly anajikuta uso kwa uso na Malaika – kumbe wanajuana! Ila mambo yanageuka ghafla baada ya Malaika kumpiga kofi :flushed:. Wakati huo huo, Tima na Ritha wanashikana koo juu ya watoto wa Tima :exploding_head:. Nelly naye anabaki kusikiliza Abby akimuomba msamaha kwa kutokuwa mume bora. Mapenzi, vuta nikuvute na siri zinapamba moto zaidi!
Mqhele Akiri Kumdhulumu Mkewe, Mandisa Achoma Hela – The Wife Image : 2244
Mqhele Akiri Kumdhulumu Mkewe, Mandisa Achoma Hela – The WifeDrama ndani ya familia ya Zulu yazidi kupamba moto! Mqhele anakutana na kikao cha kaka zake na kuulizwa kama kweli amempiga mkewe. Anakiri makosa yake na anadhibiwa vikali. Wakati huo huo, Ngoba anajivunia mbele ya kaka zake kuhusu mahusiano yake ya siri na mke wa Kamishna — uhusiano uliowawezesha kufanikisha tukio la uporaji wa kasino. Lakini bila kujua, mpenzi wake Mandisa anasikiliza kwa hasira kali… na uamuzi wake ni wa kushangaza: anachoma hela hizo wakati tayari wamemuita Kamishna aje kuchukua sehemu yake. Je, familia hii itaweza kupona baada ya usaliti huu mkubwa? Usikose The Wife kwenye Maisha Magic Bongo!
Razia Afumaniwa na Kipimo cha Mimba – JIVU Image : 2243
Razia Afumaniwa na Kipimo cha Mimba – JIVUDrama yazidi kupamba moto ndani ya JIVU! Fahad anamkaba Razia baada ya kugundua kipimo cha ujauzito chumbani kwao — kwa nini hakumwambia kama ana mimba? Wakati huo huo, Sikujua anamfungukia mpenzi wake Mchuma kuhusu tukio la kubakwa lililompelekea kupata ujauzito. Je, ukweli huu mzito utavunja uhusiano na familia nzima, au kufungua mlango wa maafa makubwa zaidi? Usikose JIVU kwenye Maisha Magic Bongo!