Logo
channel logo dark

Jua Kali

160Tamthilia16

Siri ya Naira na Frank – Jua Kali

Habari
16 Machi 2022
Siri ya Naira na Frank inaweza kugunduliwa!
Untitled design (18)

Kwa muda mrefu Frank amekuwa akimchezea Naira na pia kumtesa. Kwa ukweli Naira, alianza kumpenda Frank lakini Frank alikuwa akimtumia tuu. Penzi lake Frank lilikuwa kwa Maria. Mwanakondoo Maria nae alikuwa na shida yake, huku pembeni alikuwa akitembea na Thomas pamoja na kijana wake, Felix. Pale mambo yalipomshinda, aliamua kwenda kwa Frank.

Mapenzi kati ya Maria na Frank yazidi kukolea, lakini mwanakondo mwenzae, Lukas bado anaumia. Mwaka jana kama unakumbuka, Lukas alitaka kumvalisha Maria pete mbele ya waumini wenzao lakini hakuweza kwasababu Maria alikataa kumuoa juu yay eye kutokuwa na pesa.

Huku nyumbani kwa Frank, moto uliwaka baada ya Anna kuwaambia watu wote nyumbani kwamba Frank alikuwa anatembea na Naira. Kwa sababu akili ya Anna bado ijakaa sawa, watu wengi wanadhani kwamba amechanganyikiwa. Lakini ukweli ni kwamba, Naira alikuwa anatembea na Frank. Kwa sasa, Bill anataka kumuoa lakini amsikia Naira akisema kwamba anahisi ana mimba. Bill aanza kujiuliza kwani ni ukweli ama? Baada ya kumshirikisha Frank kimawazo kwamba anahisi kwamba Naira ana mimba Frank aanza kupata wasiwasi kwamba siri yake na Naira itagunduliwa. Je itakuaje?

Siri ya Naira na Frank – Jua Kali

Maria atagundua kwamba Naira amebeba mimba ya Frank? Tuambie hapo chini

Ndio70%
Hapana14%
Naira hana mimba16%

Usikose kuangalia #MMBJuaKali kila Jumatano hadi Ijumaa saa 3:30 usiku ndani ya DStv chaneli 160!

Kwa mengine zaidi 👇👇