Logo

Jua Kali ya teuliwa ndani ya tuzo za Zikomo

Habari
29 Septemba 2022
Tusaidie kuwapigia kura Jua Kali!
MMB Juakali ShowpageBillboard 1600x800

Zikomo Awards ni tuzo kubwa ndani ya nchini Zambia, inaangalia watu bingwa ndani ya sehemu ya burudani na sanaa kadhalika. Mwaka huu, Zikomo Awards zilizidisha tuzo zao ili kuweka pamoja tuzo za wanamitindo, muziki na watu wote wanaofanya kazi za hisani ndani ya bara la Afrika.

Mwaka huu, Zikomo Awards zitakuwa ndani ya mji wa Lusaka, Zambia. Kulikuwa na makundi ya kuzidi ishirini ya uteuzi tofauti na kipindi kinachopendwa sana ndani ya Maisha Magic Bongo cha Jua Kali kilifanikiwa kuteuliwa ndani ya kategoria ya BEST MOVIE/SERIES OF THE YEAR IN AFRICA (Kipindi bora cha tamthilia ndani ya bara la Afrika).

Jua Kali ni kipindi cha Maisha Magic Bongo kilichoanza kuonyeshwa ndani ya chaneli ya DSTV 160, Januari mwaka 2021. Kipindi hiki kinausu Professor Bili ambaye ni bingwa wa kupiga hesabu zake huku akiwatumia watu mbalimbali katika michezo yake michafu. Mpambe wake Thomas, moja ya wanafunzi wake vipanga. Direkta wa Jua Kali ni Leah Lamata.

Tunapenda kuwapa hongera kundi nzima la #MMBJuaKali kwa kazi nzuri na pia unaweza kubonyeza hapa kuwapigia kuru: https://www.zikomoawards.com/vote/!

Zaidi kuhusu Zikomo Awards: