Ndoa ya Michael na Mary inachangamoto nyingi sana. Ukiacha matatizo zao wenyewe, kama mme na mke kuna nyingine zaidi. Kuanzia mama Michael, Vivian, michepuko ya Michael na shida ya kupata mtoto, majanga yamewakumba.
Baada ya kugombana na Michael na kumwagia maji, Michael alimua kuondoka kwenye nyumba yao ya ndoa kwa nia ya kuachana na Mary. Kwa jinsi Mary alivyokuwa anampenda Michael, alikataa kabisa kumwacha aaondoke na alimfuata kwa mama yake.
Baada ya kuanza kuishi na mama yake na Michael, ndoa yao ilizidi kudidimia na Michael akaendelea kuwa na nyumba ndogo mbali mbali. Mary alienda kwa hao wanawake wake ili kuwaonya wasiwe karibu na mme wake. Hili jambo halikumfanya Michael aachana na hao wanawake, na Mary aliamua kuwa ndio muda sawa kumwambia Michael kwamba anaujauzito wake.
Sio kila mtu alikuwa amefurahi kusikia Mary ana mimba na Vivian alikuwa anataka kujua ni kweli kama hii mimba ni ya Michael. Katika uchunguzi wake, Vivian aligundua kwamba Mary nae alikuwa na mtu wake wa pembeni na sasa hatujui huu ujauzito ni wa wanani?
Usikose kuangalia vipindi vya #MMBJuaKali kila Jumatano hadi Ijumaa saa 3:30 usiku ndani ya DStv chaneli 160!
