channel logo dark
Season 14
channel logo dark

Huba

160Tamthilia16

Happy apata wageni – Huba

Habari24 Agosti 2021
Hatimaye Chidi apata nafasi yakukutana na familia ya mke wake.
Screenshot 2021 08 16 at 13

Happy alikuja mjini kutafuta kazi, na kwa bahati nzuri Tim ana Devi walimuamini na kumpa kazi nyumbani kwao. Tangu alivyo fika mjini mambo mengi yamebadirika. Alikutana na Chidi, wakapendana na hatimaye walifunga ndoa.

Baada ya kufunga ndoa, Happy alikuwa bado anajihisi mpweke sana. Kwenye harusi, ni familia ya Chidi tuu iliyokuwepo na kwa upande wake yeye hakukuwa na mtu yoyote. Hili jambo lilimsikitisha sana Happy na akamuomba Chidi asafirishe baadhi ya familia yake ije Dar.

Kwa bahati nzuri, baba yake na mdogo wake walipanga safari ya kuja Dar es Salaam. Walivyofika Dar es Salaam, walibiwa mabegi yao na wakapoteza mawasiano na pia walipotea njia ya kwenda kwa Happy.

 

Kwa bahati nzuri, walikutana na Nicole na Nicole akawapa sehemu ya kulala. Baada ya kupokewa vizuri, baba yake Happy aliamua kumuibia Nicole na ndio hapo alipowatimua toka kwake. Je Happy ataweza kuwapata kabla hawajapotea zaidi?

Usikose kuangalia kipindi kipya cha #MMBHuba kila Jumatatu hadi Ijumaa saa 3 kamili usiku ndani ya Maisha Magic Bongo, chaneli 160!