Logo

‘Bendera nyekundu’ za kuepuaka ndani ya mapenzi – Maisha Magic Bongo

Habari
24 Februari 2023
Orodha ya baadhi ya vitu kuepuka ndani ya mahusiano mwezi huu wa mapenzi
Article

Kuna baadhi ya mahusiano ndani ya vipindi vya Maisha Magic Bongo ambayo yanatuacha tukijiuliza kwanini bado hao wanandoa bado wapo pamoja? Soma hapo chini kujua ni vitu gani vya kuviepuka ndani ya mapenzi

Kuachana kila mara (Regina na Edu)
Ingawa Edu na Regina wana mtoto pamoja na wanadai kupendana, mahusiano yao wamekuwa hayaeleweki na kila mara wanachana na kurudiana. 

Kutoaminiana (Doris na Roy – Huba)
Baada ya Roy kutofanyikiwa kuchagua kati ya Nandy na Doris, aliamua kuwaoa wote wawili. Kwa sasa hivi, baada ya Nandy kurudi mjini Roy azidi kuficha mahusiano yake na Nandy kwa Doris wakati pia akimficha Nandy kuhusu mahusiano yake na Doris.

Uongo (Maria na Frank)
Ingawa Maria alivishwa pete na Frank, bado anamahusiano ya kichini na Thomas. Sasa itakuaje baada ya kuamua kufunga ndoa wakiwa bado na uongo ndani ya mahusiano yao.

Usikose kuangalia tamthilia zote uzipendazo ndani ya DStv chaneli 160! Jibu swali hilo hapo chini 👇