Dr Kumbuka alizaliwa Dar es salaam, Tanzania. Katika familia ya Watoto watatu na yeye ni mtoto wa pili. Amesoma elimu yake ya msingi shule iitwayo kipawa iliyopo uwanja wa ndege, Dar Es salaam na akaendelea na masomo yake ya sekondari Kisaki sekondari Morogoro.
Baada ya hapo akajiunga na chuo cha Utumishi wa umma Tanga. Na kupata diploma ya record.hakuishia hapo alisoma chuo cha sana ifakara na kuibuka kidedea shindano la mshehereshaji bora ktk shughuri mbali mbali za serikali na watu binafsi kama MC.
Pia alishinda shindano la mtaa kwa mtaa lilokuwa likifanywa na radio times fm nakuibuka kidedea na kupata kazi utangazaji ktk radio times fm iliyopo Dar Es salaam kawe beach kwenye kipindi cha mitikisiko ya pwani. Ndoto zake ni kuwa mshehereshaji Mkubwa ktk shughuri mbali mbali za kijamii na kuelimisha vijana na kumiliki kituo cha Tv.
Usikose Mizani ya Ushambenga kila Jumatano saa 1 Usiku