Logo
Divas & Hustlas
channel logo dark

Divas And Hustlas

160Lifestyle16

Dr Kiagho Kilonzo azindua vipindi vipya ndani ya Maisha Magic Bongo

Habari
14 Julai 2023
Wimbi na Divas & Hustlas za zinduliwa na Multichoice Tanzania
Article

Jioni ya tarehe 12 August 2023, Multichoice Tanzania ilifanya uzindulizi rasmi wa #ContentShowcase2023 ndani ya hoteli ya Delta, jijini Dar es Salaam. Ndani ya showcase hii walizindua vipindi viwili vipya vya viwili.

#MMBWimbi kilichoanza tarehe 3 Julaicha. #MMBDivasAndHustlas kilichoaanza tarehe 13 Julai. Kipindi cha #MMBWimbi ni tamthilia moto inayohusu wivu, tamaa, mapenzi na migogoro ya kila aina , ikitawaliwa zaidi na usaliti wa hali ya juu.

Kundi la Wimbi ndani ya showcase

 #MMBDivasAndHustalas ambacho ni kipindi cha uhalisia,  Wabunifu kwenye tasnia ya burudani wanapambana kukuza brand zao huku wakikumbwa na changamoto mbali mbali kwenye mishe mishe zao na maisha Yao binafsi. Tutapata nafasi ya kuona undani wa maisha yao ya kila siku

Kundi la Divas & Hustlas ndani ya showcase

Uzinduzi huu ulihudhuriwa na mgeni rasmi,Katibu mkuu wa Bodi ya Filamu Tanzania  Dr Kiagho Kilonzo, pamoja  na wadau wengi wa sekta ya Sanaa, Habari wengine chungu nzima  ikiwemo wasanii  maarufu wa tamthilia zetu za Maisha Magic Bongo .  

Mgeni Rasmi: Dr Kiagho Kilonzo

Mkurugenzi mtendaji wa Multichoice Tanzania, Jacqueline Woiso  alikaribisha wageni wote na pia kuzungumza kuhusu mipango ya Multichoice Tanzania na lengo kubwa la kukuza tasnia ya television na filamu nchini. 

Mkurugenzi mtendaji wa Multichoice Tanzania: Jacqueline Woiso

Maisha Magic Bongo tunaahidi kuendelea kuwaletea burudani kabambe bila kikomo na tutazidi kutoa mchango wetu katika kukuza sekta Filamu nchini Tanzania.

Endelea kufurahia vipindi vyetu kila siku Zaidi usikose  cha #MMBWimbi kila Jumatatu hadi Ijumaa saa 4 usiku na #MMBDivasAndHustlas kila Alhamisi saa 1 usiku kupitia DStv chaneli 160!