Logo
channel logo dark

Slay Queen

160Drama16 V

Bahati Mbaya Ya Alice – Slay Queen

Habari
09 Septemba 2020
Hakuna kitu Alice ana hamu nacho kama mwanamume anaye mpenda vyema
Alice Article Slay Queen

Tangu tulivyo kutana na Alice kwenye msimu wa kwanza wa #SlayQueenTZ alikuwa ni dada mpole sana. Tumeona jinsi urafiki wake na Mamy ulivyo kuwa kutoka kuwa madada na sasa hivi wanawake wanaojitegemea.

Kama sisi wengi, Alice ni mtu anayependa mapenzi sana na kila akikutana na mwanaume anayempenda nikama hadithi ya kwenye vitabu vya mapenzi kwake. Alice ni mtu rahisi kumganda mtu anaye mpenda hata kama hilo penzi hali rudishishwi kwake. Tuliona mfano jinsi alivyo mpenda Derrick Kasongo ingawa Derrick alikuwa na Agnes. Alivyo sikia Derrick alitaka kumvisha pete Agnes, alienda kwenye sherehere kudai anampenda.       


Baada ya aibu aliyo pata kwenye sherehe ya Agnes na Derrick. Alice aliamua kuachana na wanaume na kujipenda mwenyewe. Wakati huu ulikua mzuri kwake, alianza kupendeza tena na akaanza kujaa ujasiri. Wakati huu pia aliutumia ku kuza urafiki wake na Mamy na Mamy akamtambulisha kwa Brian.
Mapenzi kati ya Brian na Alice yalianza vizuri na wakajikuta wanaishi kama mume na mke. Kwa muda huwo mambo yalikuwa hayendi vizuri kwa upande wa Mamy, ajikuta anamwonea gere rafiki yake. Hizo hisia zilimfanya amlazimishe Alice amuunganishe Mamy na rafiki yake Brian. Hilo jambo Alice akataa na kwa hasira Mamy aamua kuchukua Brian awe wake.

Ingawa Brian ameamua kumfanya Mamy mchepuko wake, na kumtimua Alice toka kwenye nyumba yake bado hajaamua ni nani atamuoa.   
Endelea kufuatilia tamthilia yetu ya  #SlayQueenTZ kila Jumatano mpaka Ijumaa saa 3:30 usiku, na Marudio kila Jumamosi saa 7:30 mchana ndani ya Maisha Magic Bongo chaneli 160.