Logo
Slay Queen SP Billboard
channel logo dark

Slay Queen

160Drama16

Siri 6 zilizogunduliwa ndani ya #SlayQueenTZ mwaka huu!

Habari
31 Decemba 2020
Tunakuletea siri zote kali zilizo lipuka ndani ya #SlayQueenTZ ndani ya mwaka 2020!
20201231 084739

1. Uhusiano kati ya Mzee Kasongo na Julieth

Baada ya Mzee Kasongo na Julieth kuanza mahusiano, Juleth aligundua kwamba Mzee Kasongo ni baba yake na rafiki wake wa karibu, Evelyn. Kwa muda Mzee Kasongo na Julieth walijaribu kuficha lakini siri zote zilisha baada ya Mama Kasongo kuwafuma na pia hiyo siri kusabishia Mama Kasongo kifo.

2. Uhusiano kati ya Derrick na Mami

Ingawa Derrick alikuwa kwenye uhusiano na Agnes na walkuwa tayari kufunga ndoa, bado pembeni aliendea na uhusiano na Mami. Hiis siri iliwekwa wazi kwenye siku ya harusi ya Derrick na Agnes.

3. Baba ya mzazi wa Julieth

Baada ya Dk. Kileo kukutana na mama yake Julieth kwenye msiba wa Mama Kasongo, ajifunza kwamba walivyofanya mapenzi zamani, matokeo yake ilikuwa mtoto wa kike na huyo mtoto alikuwa Julieth.

4. Uhusiano kati ya Aniseta na Ben

Ingawa Aniseta alikuwa na mahusiano na bosi wake Mzee Kasongo, pia alikuwa na mahusiano na mume wa Restuta, Ben. Baada ya estuta kugundua kwamba Aniseta ana ujauzito na kufikiria kwamba hiyo mimba ni ya Ben, alimwambia Ben. 

5. Christ kutekwa

Chris na Nana walivyoanza mapenzi, mama yake Nana hakupenda kwasababu Chris ni maskini. Mama yake Nana alimlazimisha mwanae aanze mahusiano na Dk. Kileo. Tatizo lilikuwa kwamba ingawa Nana alikuwa na Dk. Kileo, moyo wake bado ulikuwa kwa Chris na akaendelea na mahusiano na Chris. Dk. Kileo alivyogundua aliona wivu na aliamua kumteka Chris ili asionane na Nana.  

6. Aniseti kuhusika kwenye utekaji wa Julieth

Baada ya Restuta kuweka tracking kwenye simu ya Aniseta, aligundua kwamba Aniseta ndiye aliyemteka Julieth.

#SlayQueenTZ na Maisha Magic Bongo inapenda kukutakia heri ya mwaka mpya. Usikose kuburudika na kipindi cha #SlayQueenTZ kila Jumatano hadi Ijumaa saa 3:30 usiku ndani ya chaneli 160!