Logo

Dr Desire amchague nani? - Karma

Habari
19 Januari 2021
Dr Desire amekwama, kati ya Lorenzo, Tadei, Raheem na Derrick
Screenshot 2021 01 15 at 17

Baada ya kuchua muda na kurudi nyumbani kwa mama yake, Dr Desire alifikiria kwa jinsi gani alitaka maisha yake yazidi kusonga mbele. Kwasababu, ukimwona kwa njee ni rahisi kuona kwamba ni mwanamke aliye kamilika na hamna chechote alichopungikiwa. Lakini ukweli ni kwamba bado anatafuta mtu wa kumpenda na kumdhamini milele na amekwama kati ya hawa kaka wanne.

 

  1. Lorenzo

Lorenzo ni mtoto wa tajiri na ni kweli Desire anampenda sana Lorenzo. Lakini tatizo lina kuja hapo ambapo Desire anashindwa kumuamini Lorenzo. Lorenzo ni mwanaume aliyezungukwa na wanawake wengi na Desire ana wasiwasi kwamba Lorenzo anaweza kumletea maradhi ya moyo na pia maradhi ya mwili.

  1. Tadei

Tadei na Dr desire wana historia ndefu sana tangu walivyokuwa wadogo na Desire anampenda sana Tadei. Tatizo kubwa kwake Tadei ni hali yake ya uchumi. Kwa jinsi Desire alivyotoka kwenye umasikini, hataki kurudi tena huko. Anataka mwanaume atakae weza kuhudumia na kumpa maisha bora.

  1. Raheem

Raheem na Desire wana mahusiano magumu sana, kipindi Desire alivyokuwa anasoma alikutana na Raheem. Kwasababu Desire hakuwa na pesa ya kujisomesha alizamiswa kuanza kujiuza mwili ili aweze kulipia ada shuleni. Baada ya kumaliza shule Raheem akazidi kumsaliti Desire na kumlazimisha awe naye kimapenzi.

  1. Derrick

Derrick na Desire walikutana kazini ambapo walianza kuzoeana. Ingawa kipindi Derrick alivyo kutana na Desire alikuwa tayari na mahusiano na Misa na walikuwa tayari wanaishi pamoja. Desire anampenda sana Derrick kwasababu Derrick ni msomi, tajiri na ana mzutio kwake.

Desire amekwama na anafikiria kwa makini san ani nani amchague. Fanya kipima joto chetu “Msahidie Desire kuchagua mpenzi” kujua ni nani unafikiri atamfaa Desire. Pia, usikose kuangalia #KarmaTZ kila Jumamosi na Jumapili saa 3 usiku ndani ya chaneli 160.