Logo
channel logo dark

Jua Kali

160Tamthilia16

Title: anna avishwa pete! – Jua Kali

Habari
22 Aprili 2021
Baada ya kupata bahati mbaya kwenye mapenzi hatimaye Anna avishwa pete.
tony eight media wcSJB1SdDkU unsplash

Baada ya kuumizwa na George na kugundua kwamba George alikuwa na mke na pia watoto wawili. Anna aliamua kuachana na George na aendelee kivyake.

Inaonekana kama katika utulivu wake, Anna ndipo alivyoanza kupata bahati ya mapenzi. Kwanza ilikuwa Michael. Michael kwa ghafra aliamua kumwambia Anna kwamba anampenda na angependa wawe Pamoja, lakini Anna alikuwa anamuona Michael kama kaka yake kwa hilo alikataa kabisa.

Baad ya Michael, Dominic aliingia ndani ya picha. Dominic ni mwanaume mpya, ni mbwana mzuri san ana mtanashati sana. Alivyogusa tuu ofisini kwa Anna alisema alikuwa mekuja kwa kisa ya kumuona Anna. Alikuwa mfuata Anna kibiashara na baada ya kukutana na Anna alivutiwa kwake na kumpenda na walianza mahusiano.

Baada ya muda kidodo Dominic aliamua kumvisha pete, akidai kwamba anampenda. Marafiki zake wote na Anna walifurahi sana ila tatizo ni mama yake Anna. Mama Anna anadaikwamba Anna na Dominic wanaenda kwenye mapenzi kwa mwendo wa kasi sana. Juzi juzi tuu, Anna alikuwa anamlilia George na leo hii yuko tayari kumuoa mtu amabaye amemjua kwa muda mfupi tuu. Je Anna amepata penzi lake la daima au amsikilize mama yake na awe makini?