Logo
channel logo dark

Jua Kali

160Tamthilia16

Penzi linaumiza sana – Jua Kali

Habari
07 Mei 2021
Anna, Naira na Felix wafanye nini?
Screenshot 2021 05 07 at 09

Mapenzi ni matamu lakini yanaweza kuumiza sana, na wiki hii tumeona jinsi Anna, Naira na Felix walivyoumizwa na haya mapenzi.

Anna

Baada ya kuachana na George na kukutana na Dominic, Anna alikuwa tayari kuolewa nae. Ingawa mama yake alimwambia awe makini kwasababu hakumjua Dominic, Anna hakusikiliza. Kwenye siku yao ya harusi Dominic hakuja na alimwacha, na kumwambia kwamba hampendi na muda wote alikuwa ana mahusiano na rafiki wa karibu wa Anna.

 

Naira

Naira anampenda kaka Frank sana, lakini Frank anamtumia tuu. Amejaribu kila kitu kumpata Frank kuanzia jinsi anavyovaa na kumsingizia mimba lakini bado Frank hamtaki.

 

Felix

Felix anampenda sana Maria mpaka wakawa na mpango wakufunga ndoa. Maria yeye kumbe muda wote alikuwa anamtumia Felix na alikuwa na mambo yake pembeni. Kwenye siku ambayo alikuwa akutane na familia ya Felix, Felix na Stella awaligundua kwamba Maria ndie mchepuko ya baba yake Felix, Thomas. Tangu hapo moyo wa Felix ulivunjika sana.

 

Je unafikiri Anna, Naira na Felix wapona na maumivu ya moyo? Usikose kuangalia #MMBJuaKali kila Jumatano hadi Ijumaa saa 3:30 usiku ndani ya chaneli 160 ya DSTV.