Logo
Huba
channel logo dark

Huba

160Tamthilia16

Ni nani umefurahia zaidi kumuona tena? – Huba

Habari
21 Mei 2024
Nicole na Devi warudi ndani ya tamthilia ya #MMBHuba.
Huba

Baada ya miezi bila kujua Nicole na Devi wako wapi, hatimaye wapenzi wa Huba wamepata walichokuwa wakiomba. Wiki iliyopita tuliiona jinsi Nicole alivyorudi na pia jinsi Devi alivyorudi ndani ya tamthilia hii.

Nicole aliondoka baada ya kubeba mimba na aliachana na Jude, jambo hili lilimvunja moyo Jude na Jude alijikuta mikononi mwa Doris. Kwa sasa Nicole amerudi tena bila mimba wala mtoto. Je, itakuaje?

Devi naye alipatwa na ajali mbaya kabla ya kuondoka. Ajali hii ilitokea baada ya kumfumania mama yake, Tesa, akiwa pamoja na rafiki yake wa karibu, Roy. Baada ya kuwa mahututi kwa muda mrefu, alisafirishwa Afrika Kusini kwa matibabu. Baada ya mama yake kupoteza imani kwamba yupo hai, Devi amerudi. Je, itakuaje?

Kumbuka kujiunga na #MyDStv App kufuatilia tamthilia ya #MMBHuba popote ulipo na pia usikose vipindi vipya kila Jumatatu hadi Ijumaa saa 3 usiku ndani ya DStv chaneli 160!

Devi na Nicole warudi ndani ya Huba

Ni nani umefurahia zaidi kumuona tena? – Huba

Huba
Nicole45%
Huba
Devi55%