Logo
Huba
channel logo dark

Huba

160Tamthilia16

Je Kibibi amuhurumie Tesa? – Huba

Habari
21 Aprili 2024
Baada ya Tesa kuachwa na Roy na kujaribu kujiua, Chidi aliamua kumsaidia na kumleta nyumbani kwake na Kibibi.
Huba

Mwaka huu umekuwa mbaya sana kwa Tesa, tangu Devi alivyopata ajali na kupelekwa Afrika Kusini kupata matibabu, Tesa amekuwa anafanya chochote kile iliawzekurudisha nyumbani.

Wakati wa kipindi hiki Tesa amekuwa ndani ya mahusiano na Roy, na mahusiano yao yakuwa mateso makubwa kwa Tesa. Baada ya kutapeliwa na mchungaji na kupoteza pesa zake zote Roy aliamua kuachana nae, ili aende kumtafuta mpenzi wake wa dhati, Nandy.

Baada ya kuachwa na Roy na pia kutokuwa na pesa ya kwenda kumuona mwanae, Tesa alijaribu kujiua. Aliamua kuacha kula kwa muda mrefu na aliishia mahututi hospitalini. Baada ya Chidi na Kashaulo kupata taarifa ya Tesa, waliamua kumsaidia na Chidi alimpeleka nyumbani kwake na Kibibi ili aweze kuponea huko. Tatizo kubwa ni kwamba Tesa na Kibibi wamekuwa maadua wakubwa kwa miaka mingi sana. Kabla ya Kibibi kuolewa na mwanae Devi, mahusiano yao hayakuwa mazuri lakini ndoa yake kwa Devi ilizidisha uadui zaidi.

Huba
Tesa na Kibibi - Huba

Je Kibibi amruhusu Tesa akae nyumbani kwake?

Ndiyo91%
Hapana9%

Fuatilia kipindi cha #MMBHuba kila Jumatatu hadi Ijumaa saa 3 usiku ndani ya Dstc chaneli 160, Maisha Magic Bongo. Pia jiunge na maongezi kupitia kurasa zetu za mitandao ya jamii: Instagram, X, Tiktok, Facebook na YouTube.  

Kwa Zaidi: