Logo
Huba S12 BB
channel logo dark

Huba

160Drama16

Wake wenza walimpendeza nani zaidi mwaka huu? - Mazuri ya 2023

Habari
07 Decemba 2023
Kati ya Nguzo, JB na Prof Bill nani alipendezwa na mke zaidi ya mmoja mwaka huu?
Article

Ndani ya mila na desturi ya waafrika wengi, uke wenza sio kitu kigeni. Kwenye tamthilia zetu, tunapambana sana na wanaume wenye wake zaidi na mmoja na kila siku tunaona jinsi wanavyoendelea na maisha yako nyumbani.

Nguzo (Mpali)

Mzee Nguzo amekuwa akiongoza kwa wake wengi ndani ya Maisha Magic Bongo. Hivi karibuni ameliamua kuwapeleka wake wote kwenye likizo baharini. Hii likizo iliishia vibaya baada ya wake zake kupigana. Watu wengi wamekuwa wakisema kwamba bwana Nguzo ana mke mmoja anayempenda zaidi ya wote wengine, je unfikiri huo ni ukweli?

JB (Huba)

Swala lake la ushirikina limemfanya JB awe na tamaa sana. Tamaa yake haishii kwenye pesa tuu, imeingia hadi kwenye maisha yake ya kimapenzi. Kwa sasa hivi JB ana wake wawili, Happy na Tima. Baada ya kumhamisha Happy kwenye nyumba aliyokuwa akikaa na Tima, moto uliwaka nyumbani. Je hii kasheshe itaishaje?

Prof Bill (Jua Kali)

Kwa jinsi Prof Bill alivyokuwa akiheshimiwa ndani ya jamii yake, kitu cha mwisho mtu yeyote alikuwa akifikiria ni kwamba ataishia na wake wawili. Baada ya siri yake kuhundulik kwamba yeye ndiye baba mzazi wa mtoto wa kijakazi wake kwa miaka, Zai, alifanya muamuzi wa kuchukua wake wawili. Sasa Mrs Bill pamoja na Zai waendelea kukaa kwenye nyumba moja kama mtu na bosi wake na pia kama wake wenza.

Wake wenza walimpendeza nani zaidi mwaka huu? - Mazuri ya 2023

Kati ya hawa watatu, ni nani anapendezwa na wake zake?

Poll
Nguzo (Mpali)65%
Poll
JB (Huba)6%
Jua Kali
Prof Bill (Jua Kali)29%

Usikose kuguatilia tamthilia uzipendazo kila siku ndani ya DSTV chaneli 160. Pia jiunganishe na #MyDStv app kwa zaidi