Logo
Huba S12 BB
channel logo dark

Huba

160Drama16

Sababu tatu zakutorudiana na ex wako – Huba

Habari
20 Oktoba 2023
Je unawezakurudiana na ex wako kama Kibibi na Chidi?
Huba

Kuvunja uhusiano na mtu unayempenda mara nyingi sio rahisi, na ni kawaida kuwa na mawazo ya kurejesha uhusiano na mpenzi wa zamani. Baada ya Chidi na Kibibi kuachana kwa miaka sasa, wameanza ukaribu tena. Tumetoa sababu tatu kwanini wazo zuri kurudiana na ex wako:

Haujui kwa uhakika kama mambo takuwa tofauti mkirudiana:

Kuna sababu kubwa Chidi na Kibibi waliachana, na sasa hivi maisha yao ni tofauti sana. Walivyoanza mahusiano, Kibibi na Chidi walikuwa wanafanya kazi pamoja na wanakaa uswazi, sasa hivi Kibibi amempita Chidi kimaisha baada ya kupata pesa na mahusiano yao hayawezi kuwa kama zamani.

Hofu ya Ukiwa mpweke:

Baada ya Kibibi kuachwa na Devi na Chidi kuachwa na Happy, wote wamejikuta wakiwa wapweke. Kwa hiyo sababu wanaweza kuwa wanatumiana kuliko kupendana.

Kuwa pamoja kwaajili ya mtoto:

Kibibi na Chidi wana mtoto mmoa, Angel. Kwasababu wamezoeana na labda wanataka kuwa pamoja kama familia. Lakini, kama hamna penzi la kweli wanaweza kuishia kumuumiza mtoto wao.

Huba
Chidi na Kibibi - Huba

Je umekubali kwa Kibibi na Chidi kurejesha huba lao?

Ndiyo16%
Hapana84%

Endelea kufuatilia #MMBHuba kila Jumamatu hadi Ijumaa saa 3 usiku ndani ya #MaishaMagicBongo na jiunganishe na #MyDStv App kupata burudani zote popote ulipo.