Logo
Huba S12 BB
channel logo dark

Huba

160Drama16

Mapenzi au pesa? – Huba

Habari
06 Novemba 2023
Ungechagua tatizo la nani kati ya Doris na Happy?
Huba

Siku hizi mapenzi yakuja na masharti mengi, kuna watu wanaotaka mapenzi ya dhati kama Doris na watafanya lolote kuyapata. Wakati pia kuna wengine wanaotumia mapenzi kama suluhisho ya matatizo yote ndani ya maisha yako kama Happy.

Doris

Toka mwanzo Doris ni aliyekuwa akiamini mapenzi ya dhati. Miaka nenda na miaka rudi tumekuwa tukiangalia jinsi alivyokuwa akimpigania Roy. Kuanzia kwa Nandy na hatimaye kwa Tesa. Baada kukutana na Abby, Doris alijikuta amepoza akili kabisa na mapenzi yamemkolea kuzidi kipindi alipokuwepo na Roy. Amejikuta akiwa analipia kila kitu na kufukisha hatua ya kumuazima Abby pesa. Mama yake amejaribu kumuonya lakini kwa jinsi huba ya Abby lilivyo mnogea, Doris haoni au hasikii kabisa. Sasa itakuwaje? Doris ana moyo mzuri na malengo yake ni ya halali, akipenda anapenda sana na kwa dhati, lakini hilo penzi lake lina mponza kila siku. Tuambie hapo chini kama unafiki ni bora kuwa mtu wa kupenda bila kikwazo kama Doris? Au ni bora usipende kabisa kuepuka moyo wako usivunjike?

Huba
Doris

Tuambie hapo chini kama unafiki ni bora kuwa mtu wa kupenda bila kikwazo kama Doris?

Ndiyo6%
Hapana94%

 

Happy

Tulivyokutana na Happy kwa mara ya kwanza, alikuwa dada mpole aliyekuwa kijakazi wa Tima. Baada ya muda, Happy aliolewa na Chidi, mwanaume mwenye hali ua chini ki maisha. Baada ya kua hana na Chidi, Happy alijikuta mikononi kwa JB, mwanaume tajiri anayejiweza. JB alimpandisha cheo Happy na kumpa maisha mazuri, lakini Happy sio mke pekee wa JB, yupo pamoja na Tima. Uke wenza sio tatizo pekee ndani ya ndoa ya Happy na JB. JB anamzidi umri mwingi sana Happy na mtu yeyote anaweza kuona kama penzi lao sio la dhati kabisa. Je ni bora kuwa na mtu tajiri kama JB kuliko kuwa na penzi la dhati?

Huba
Happy

Je ni bora kuwa na mtu tajiri kama JB kuliko kuwa na penzi la dhati?

Ndiyo0%
Hapana100%

 

Endelea kufuatilia kipindi cha #MMBHuba kila Jumatatu hadi Ijumaa saa 3 usiku ndani ya #MaishaMagicBongo na usipitwe na lolote kwa kujiunganisha na #MyDStv App.