Logo
Huba S12 BB
channel logo dark

Huba

160Drama16

Bendera nyekundu za Abby - Huba

Habari
11 Novemba 2023
Nani atawaokoa Nelly na Doris?
Huba

Tangu Abby alivyoingia ndani ya #MMBHuba, wanawake wengi  walimpenda lakini Doris alikuwa wa kwanza kumkamata roho, na baada ya kukataliwa na Fei alijikuta mikononi mwa Nelly wakati bado alkuwa na mahusiano na Doris.

Watazaji wa #MMBHuba weshatoboa siri kubwa ya Abby na siri hiyo ni kwamba, yeye ni tapeli mkubwa. Alimtaka Doris baada ya kuona kwamba ni mwanamkwe anayejitambua kimaisha na alimfuata Nelly baada ya kushindwa na ujanja wa Fei. Nelly na Doris bado wenogewa na mapenzi na wakosa kuona "warning signs" za utapeli wake. Hapo chini tuna toa bendera tatu za hatari zilizopitwa na Doris na Nelly.

 

1. Abby hana pesa ya kulipia nguo

Mara ya kwanza ya Abby kumtoa Doris njee alimpeleka madukani kununua nguo na bili ililetwa hakuweza kuilipa ba Doris ndiye aliyeishia kuilipa.

2. Alimtaka Fei kabla ya Nelly

Kipindi chote Abby alikuwa akimfuatilia Fei, lakini kwa Bahati nzuri Fei aliona utapeli wake kwa mbali na akachana nae. Ingawa yupo na Nelly sasa hivi, mwanzoni hata Nelly alifikiri kwamba anamtaka Fei na sio yeye

3. Nyumba yake haieleweki

Baada ya kumtoa Nelly kula, alirudi nae nyumbani kwake na kwa mtu ambaye bado ni kijana na anaanza maisha nyumba yake ilikuwa ya kifahari sana.

Nelly na Abby - Huba

Unafikiri Nelly atagundua ukweli kuhusu Abby?

Ndiyo73%
Hapana27%

Fuatilia #MMBHuba kila Jumatatu hadi Ijumaa saa 3 usiku ndani ya Maisha Magic Bongo