Logo
MMB HubaSM V1 TwitterCover Generic HR
channel logo dark

Huba

160Tamthilia16

Roy hawezi kuchagua kati ya Nandy na Doris - Huba

Habari
22 Aprili 2021
Nandy arudi mjini na Roy bado anahisia kwake.
Screenshot 2021 04 22 at 14

Nandy aliamuwa kumuacha Roy kwenye siku yao ya harusi baada ya Nandy kugundua meseji kutoka kwa Doris. Doris na Roy walishawahi kuwa Pamoja na Roy alimuacha Doris kwenda kwa Nandy na baada ya Nandy kuona hizo mesaji alijua kwamba Roy alirudi kwa Doris anakaamua kutoolewa na Roy na kurudi kijijini.

Alivyokuwa kijijini, Nandy alikutana na Yakubu na akampenda na walianza mahusiano. Baada ya muda, Yakubu na Nandy waliamua kurudi mjini ili Nandy aendelee kuimba na Yakubu awe manaja wake.

Tatizo kubwa ni kwamba, baada ya kurudi mjni, alikutana na Roy na wote waligundua kwamba zile hisia za zamani bado zipo na wakajaribu kuanza mahusiano mapya. Lakini Roy alikuwa na Doris na Nandy na Yakubu, sasa ilibidi wafiche mahusiano yao.

Doris alianza kuwa na wasiwasi kwamba Roy atakuwa amerudiana na Nandy na alianza na kufanya mpango ili Roy asikutane na Nandy. Lakini Roy na Nandy wameshafika mbali, je unafikiri atachagua ni mwanamke gani anamtaka? Usikose kuangalia #MMBHuba kila Jumatatu hadi Ijumaa saa 3 usiku ndani ya Maisha Magic Bongo, chaneli 160.