Logo
MMB HubaSM V1 TwitterCover Generic HR
channel logo dark

Huba

160Tamthilia16

Happy na Chidi wafunga ndoa – Huba

Habari
21 Juni 2021
Hatimaye Chidi aamua kumuoa Happy.
Screenshot 2021 06 21 at 13

Chidi na Happy wakutana wakati walivyokuwa wakifanya kazi nyumbani kwa Tima. Chidi alikuwa wa kwanza kumpenda Happy lakini kwasababu ya historia yake ya mapenzi aliogopa kuanza mahusiano na Happy. Kipindi alivyokutana na Happy, ilikuwa baada ya mke wake wa kwanza Kibibi kutoroka na kumuacha mpweke kisa hakuwa na pesa.

Kwa sababu ya hofu ya kupoteza kazi zao, Happy na Chidi waliamua kufanya mapenzi yao kwa siri. Kwa muda mrefu, hiyo siri iliendelea lakini Happy akaanza kuona kama ilikuwa dharau kwake, kwa jinsi Chidi alivyokuwa akikataa kumuoa. Hatimaye Chidi alikubali kumuoa Happy lakini Happy alitoa masharti ya hali ya juu kwa harusi yake.

Chidi aliamua kumuoa Happy nyumbani kwa Tima. Alitafuta muda ambapo Tim ana Jude walivyopanga kutoka mjini kwenda kupumzika. Aliziba nyumba nzima na kualika watu iliwafunge ndoa mabayo Happy alikuwa anataka.

Baada ya harusi, Chidi na Happy walijaribu kuficha ndoa yao. Hatimaye kwa uoga, Happy alimwambia Tima kwamba walifunga ndoa. Hili jambo halimfurahisha Tima kwa jinsi walivyomficha ndoa, lakini alikuwa hana shida na hatimaye walipata ruhusa ya kuishi kama mumem na mke.

[youtube video]

 

Kumbuka kwa unaweza kufuatilia Huba kwa njia ya Showmax muda wowote. Bonyeza hapa kujiunga sasa hivi