actor wa shobo dundo

Shobo Dundo ni movie ambayo imewakusanya waigizaji wakali kama Stan Bakora, Kitale na Batuli ambapo ni stori yenye vitu vingi ndani yake... inaanzia pale mume anamuacha mkewe nyumbani alafu mkewe analeta mchepuko kisha mume anapigiwa simu ya msiba na kurudi nyumbani ghafla. Mengi ya mastaawa bogno na maisha yao pia unaweza kuitazama kwenye Inside Bongowood, Jumanne saa 15:30 kwenye Maisha Magic Bongo.

Part I na II zilianza kununuliwa sokoni kwa kasi na mrejesho wa watazamaji wengi ukawa ni kwamba movie ni kali, kilichotakiwa ni kupata mwendelezo wa stori yenyewe ndio maana waigizaji hawa wameamua kutoa Part III & IV.

Mkude Simba Original maarufu kama Kitale amekutana na reporter wa DStv.com na kusema mpango ulikua ni kuwapa watu burudani na ubunifu wa wachekeshaji hawa ndio maana Part 3& 4 zimeachiwa sokoni rasmi sasa hivi.

Mwigizaji Kitale amesema kwamba, rekodi za movie ya Shobo Dundo zimemuonyesha bado Watanzania wanaweza kununua kazi za nyumbani kwa kiwango kikubwa ndio maana ataendelea kukaza mpaka kieleweke.