Diamond Platnumz

Diamond Platnumz kajenga msikiti iliyogharimu zaidi ya milioni 30

Inawezekana umemuona mwimbaji staa wa bongofleva Diamond Platnumz akiwa kwenye maisha mazuri kuanzia nyumbani kwake mpaka usafiri anaotembelea ila hujajua kwamba amekua akifanya ibada na kumshukuru Mwenyenzi Mungu.

Kwenye exclusive na DStv.com leo Diamond kakutana na reporter Millard Ayo na kuweka wazi kwamba ni kweli amekua kwenye ujenzi wa msikiti.

Pia unaweza kujua mengi kuhusu mastaa wa Tanzania na maisha yao kwenye Inside Bongowood, Jumatano saa 18:35 kwenye Maisha Magic Bongo.

Amesema, "Msikiti nimeujenga kule Mkuyuni Morogoro ni baada ya boss wangu Tale kuniambia kwamba kuna msikiti kule Mkuyuni na watu wanaswali kwa tabu sababu Msikiti ni wa udongo, watu wanapata tabu."

Diamond akaongezea, "Tuliuvunja mpaka tukaanza mwanzo kuujenga, sasa hivi ulipofikia ni karibia kukamilika.... gharama yake mpaka kukamilika ni zaidi ya milioni 30."

Akaendelea, "Mwaka 2015 nilijitahidi kufanya vitu vingi vya dizaini hii Mwenyenzi Mungu aone kabisa inawezekana kazi yangu ya muziki sio nzuri ila natumia kufanya mambo ya msingi."

Mbali ya Inside Bongowood, unaweza kuitazama DStv Catch Up ambayo inayo burudani tele kwenye DStv Explora. Jaza fomu hii kupata Explora yako kwa urahisi:

 

Fill out my online form.