Mwanamuziki maarufu Diamond Platnumz @diamondplatnumz na mchumba wake Zari Hassani @zarithebosslady wamekumbwa na madai ya kwamba mtoto wao Tiffah, ni wa King Lawrence aliyekuwa Mpenzi wake Zari.
King Lawrence amedaiwa kupeleka kesi yake Mahamkamani na kupewa amri ya kumpeleka mtoto Tiffah akapimwe damu kubaini asilia yake ya uzazi.
Diamond na Zari hawana nia ya kujibu shutuma hizi na wanaendelea kumlea mwanao kwa mapenzi. Katika habari zingine, ilisemekana kwamba Diamond Platnumz alilipa mahari kwa familia ya Zari na kumwoa.
Tunawatakia kila la heri!
Wasiliana nasi katika kurasa yetu ya Facebook na Twitter, pia Instagram na WeChat: MaishaMagicEast