Logo

Riyama

News
10 November 2015
Penzi la Riyama na Shigera linapita mipaka, linaponya magonjwa ni penzi la milele.
Riyama Artist 234 riyama artist 2resized

Riyama ni binti mrembo sana. Anampenda Shigera na wanapanga Ndoa. Wazazi wa Shigera wanamhimiza wafanye kupimwa virusi vya Ukimwi kabla ya kufunga Ndoa.Wakipimwa, Shigera anapatikana kuwa hana virusi lakini Riyama ni mgonjwa. Hili ni jambo la kustaabisha sana kwani Riyama ni Binti Bikira na haelewi jinsi alivyopata vurisui vy a Ukimwi!

Daktari anajaribu kumwelimisha namna nyingineo mtu anavyoweza kuambukizwa virusi vya Ukimwi, kisha, anakumbuka jinsi alivyoishi na rafikiye, Dhahabu. Riyama anakata shauri ya kuwaelimisha watu juu ya kujikinga na Ukimwi. Vile vile, wazazi wa Shigera wanakomesha mipango yote ya harusi na kumtafutia Shigera msichana mwingine wakuoa lakini penzi lake la Riyama halifujiki kamwe na wanapendana hata kumzaa mtoto wa kiume!