Logo

MMBongo Movie, BHOOT!

News
07 December 2015
Sinema ya 'Swahindi Horror' leo saa Nne za Usiku hapa MMBongo!
Bhoot7Dec

Ni Hadithi inayohusu wanandoa Victor na Suzy walionunua nyumba ya ghorofa kwa bei ya chini sana.
Mwenye nyumba anamuongopea Victor kuwa ndani ya nyumba ile aliishi mwanamke aliyejiuwa baada ya kumuua mwanawe. Baada ya siku chache tu Suzy anapatwa na misukosuko ya ajabu ndani ya nyumba ile na mumewe anaamua kumuona daktari wa magonjwa ya akili kwa kudhani mkewe kachanganyikiwa, lakini mhudumu wake wa ndani anamwambia kuwa yale sio magonjwa ya akili bali kakumbwa na mzimu wa Manka.


34 bhoot7dec
Mchakato wa kutafuta tiba sahihi unaanza na vishindo vya ajabu kutokea. Fuatilia mkasa huu.


Wasiliana nasi katika kurasa zetu za href="http://maishamagiceast.dstv.com/https://www.facebook.com/MaishaMagicBongo">facebook, Twitter na WeChat.