Logo

Mchungaji wa kondoo au mbwa mwitu — Maisha Mkanda

News
02 March 2020
"My bishop defiled me".
maisha mkanda, bishop defiled me, bishop rapes girl

Watu wengi hutafuta hifadhi kanisani lakini ni vipi mchungaji wa kondoo anageuka kuwa mbwa mwitu na kupotosha wafuasi wake? Askofu Paul Mwangi ambayo ni mtumishi pekee wa kanisa iliyoko Taru, Kwale County alimnajisi mtoto wa kike nyumbani mwake. Cha kushangaza ni kwamba wazazi wa msichana huyo walikuwa wamempeleka shule ya askofu huyo na badala ya kumudhulumu mtoto huyo.

1583331707 34 screen shot 2020 02 26 at 12.17.48
0

Kulingana na msichana huyo, askofu alianza kumuambia kwamba anampenda. Halafu akamwalika nyumbani mwake na kumwambia atoe nguo. Baada ya kumnajisi msichana huyo alianza kupata infections kila wakati. Babake mzazi akaamua kumchukua na kuishi naye na akapona. Akamwambia mke wake achunguze kama kuna jambo lolote ambalo linamsumbua na hapo basi akafunguka na kusema kile pastor alimfanyia. 

"Ni bahati hana HIV lakini akijua vile ameniharibia mtoto wangu na usichana wake?" — Babake msichana

1583332674 34 screen shot 2020 02 26 at 12.21.18
0

Wakati uchunguzi ulifanywa ikapatikana kwamba wasichana wengine pia walikuwa wamedhulumiwa na askofu huyu. Claris Ajiambo ambae alikuwa mfuasi wake wa zamani alisimulia vile askofu huyo alimshawishi awache kazi yake na badala yake kufanya 'kazi ya mungu".

Gallery

Alifuata maagizo yake lakini baada ya hilo tukio Claris na mume wake waliishi katika hali ya umaskini sana. 

Lakini Claris hakukaa sana kwa kanisa hilo. Alijipa moyo na kusema hivi, "kuvunjika kwa mwiko sio mwisho wa kupita sima. Niliinuka na kwenda mbele na kujiamini". 

Maisha Mkanda airs every Sunday at 7:30 pm only on DStv 158 and GOtv 4.