Logo

King Kiba Akutana na NE-YO Nairobi

News
18 August 2015King Kiba kutoka Tanzania, aliyetuletea nyimbo kama “Mwana” na “Chekecha Cheketua” alikutana na mwanamuziki maarufu toka Marekani, NE-YO, anayejulikana kuwa mwanamuziki na mwandishi wa muziki moto moto  kama “Let me love you,” “Sexy Love” and “She Knows”.

Kiba alimkaribisha Ne-YO hapa Nairobi katika Coke Studio Africa.

AliKiba na baadhi ya wanamuziki wengine kama Wangechi (Kenya), Dama Do Bling (Mozambique), Ice Prince (Nigeria) na Maurice Kirya (Uganda) walijadiliana na NE-YO kuhusu muziki wa Afrika ambao alikubali unapata umaarufu kote duniani. Ilisemekana Ali na NE-YO wanamatumaini ya kushirikiana haswa katika kuandika na kurekodi nyimbo mpya pamoja.

King Kiba yuko Nairobi na anatarajiwa kurekodi wimbo na wanamuziki  hao katika mfumo mpya wa Coke Studio Africa msimu wa 3, utakaozinduliwa mwezi wa Oktoba mwaka huu. Alikiba yuko Coke Studio Africa kwa mara ya kwanza msimu huu.

King Kiba ameshirikiana na Victoria Kimani (Kenya na Tanzania) katika nyimbo za mash-up.Tunamkaribisha NE-YO huku Afrika Mashariki!

 

Kwa habari zaidi wasiliana nasi katika kurasa yetu ya Facebook na  Twitter, pia Instagram na WeChat: MaishaMagicEast