Logo

Kigogo cha Muziki wa Soukous, PAPA WEMBA ameaga dunia.

News
25 April 2016
Mwenyezi Mungu amtulize mahali pema peponi. PAPA WEMBA, 1949- 2016. Alikuwa kipenzi cha Afrika, Mwana wa Congo.
PapaWemba

KWAHERI YAYA, PAPA WEMBA


1949-2016


34 papawemba


Mashabiki wa Papa Wemba, mwimbaji mashuhuri wa muziki wa Soukous na densi ya Rhumba, walipokea habari za kifo chake kwa mshtuko sana jana baada ya kuzirai katika Jukwaa katika mji wa Abidjan, Ivory coast na kuaga dunia.

Papa Wemba aliyeiitwa Jules shungu Webadio alikuwa na umri wa miaka 66 wakati alifariki. Video iliyosambazwa kutoka tamasha la muziki #FEMUA inaonyesha Papa Wemba akiwa na  wanamuziki wenzake wakidensi na kuimba, kisha, alianguka na kuzirai.

Msemaji wake aliwaeleza wana habari ya kwamba, Papa wemba alikuwa ameiiingia jukwa kwa sekunde chache tu kabla ya mkasa huu kufanyika.
34 papawemba2res


Jules Shungu Wabadio alizaliwa mnamo Juni 14 1949 katika kijiji la Sukuru, Congo. Kipaji chake cha muziki kilijitokeza mapema, huku akimfuata mamake alipoenda katika sherehe au matanga, huku akitunga nyimbo zake za maombolezi au viburudisho.

Alijiunga na wanamuziki na wanabendi wenzake akiwa bado kijana chipukizi na kuunda kundi la Zaiko LangaLanga mwaka wa 1969.

Wakati huo, jukwaa la muziki katika Nchi ya Zaire ( Congo)  lilikuwa limetawalwa na wanamuziki mashuhuri kama Franco Luambo, Tabu Ley Rochereau wa Afrisa, na makundi mengine kama vile Les Grands Maquisards, Le Trio Madjesi, Bella-Bella, Thu Zaina na Empire Bakuba.

Papa Wemba alirushwa katika maisha ya umaarufu kwa ajili ya sauti yake ya kipekee iliyowavutia wapenzi wa muziki wa Soukous. Mnamo mwaka wa 1973, alibadilisha jina lake na kuwa 'Papa Wemba' yaani, Baba wa muziki wa mtindo wake, mchanganyiko wa Soukous na Rhumba.

Zaiko Langalanga walizuru mbali duniani na kuwavutia wapenzi wa muziki, sana sana, katika nchi za kiasili ya kifaransa kule Uropa. Baada ya kutoa wimbo "Yolele', Papa Wemba alitoka katika kundi la Zaiko Langalanga na Kuendelea kupambana na wanamuziki wenzake kule Congo.

Alijiunga na kundi lingine kabla ya kuunda kundi lake lingine, "Viva la Musica".  Papa Wemba alipatwa na visa vingi katika maisha yake.

 

Mnamo Februari 2003, serikali ya Ufaransa walimpata na hatia ya ulanguzi wa binadamu kutoka Zaire mpaka Ufaransa na kufungwa gerezani kwa muda wa miezi mitatu na nusu.

Nyimbo zake moto moto ni "Show me the Way", "Rail On", "Yolele" na zinginezo. Alipata kuimba pamoja na waimbaji mashuhuri wa Afrika kama bi Angelique Kidjo, Koffi Olomide, Diamond Platnumz na wengine wengi. Pata muziki wa Papa Wemba katika kipindi chetu cha #Rhumba Yatesa, kila Ijumaa saa 22:00 EAT, ndani ya DStv chaneli 158.

Mwenyezi Mungu amtulize mahali pema peponi. PAPA WEMBA, 1949- 2016.  Alikuwa kipenzi cha Afrika, Mwana wa Congo.

Wasiliana nasi katika kurasa zetu za facebook, Twitter na WeChat.