maisha magic bongo logo

Mtupwe Aamka! – JIVU

Video22 Novemba

Mtupwe hatimaye anaamka baada ya siku nyingi akiwa hajitambui kufuatia kipigo kikali alichopewa na Bi Barke — hatua inayozua maswali mengi kuhusu hatma yake na mustakabali wa uhusiano wao. Wakati huo huo, Munir anasikia kilio cha wafanyakazi wa Temboni kuhusu mazingira hatarishi ya kazi. Bila kusita, anaamuru kazi zisimame mpaka pale watakapopewa kofia ngumu za kujilinda. Uamuzi huu unaleta furaha kubwa kwa wafanyakazi, lakini pia unaashiria mwanzo wa mabadiliko makubwa Temboni. Je, hili litampa Munir nguvu mpya au litafungua mlango wa migogoro mipya?