Logo
channel logo dark

Kumi Za Wiki

160Muziki16

#WCW wetu wa wiki hii katika  Maisha Magic Bongo

Habari
26 Agosti 2020
Wanawake wamezidi kuwa juu kwenye muziki wa Bongo Flava siku hizi tunawaona kupitia vipindi vyetu Kumi za Wiki na Bass.
Kumi za Wiki WCW Article Front pic

Nyakati zimebadilika sana siku hizi wanawake wameonekana kuwa wachangamfu  katika maswala mbali mbali kiuchumi , kielimu na hata uongozi . Na leo hii tumeamua kuangazia wachache katika tasnia  ya sanaa za nchini Tanzania, tumebarikiwa na vipaji maradufu kabisaa, waaigizajji, waimbaji(wanamuziki) na mengine chungu nzima. Tuna waleta kwenu wachache watakao wakilisha wengi hivyo basi:


Linah Sanga
Mwanadada huyu jina lake kamili ni  Estelina Peter Sanga,  maarufu kama Linah  ni mwana muziki mkongwe katika tasnia ya muziki. Sauti yake nyororo  ilimuibua kwa kasi sana amefanikiwa pia kutoa nyimbo mbali mbali zili hit  na bado zinatamba mitaani kwetu kama ‘Malkia wa nguvu' Oletemba  na zingine chungu nzima .Anaendela kutamba na ngoma zake zingine nyingi tunazoziona kupitia vipindi vyetu vya muziki ndani  ya MMB  . “Tuliza Boli”, “Marry You” and “Pepea”zina endelea kuwepo ndani ya Kumi za wiki kila Iumaa saa 11 Jioni na Bass kila Jumatatu-Alhamisi saa 11 jioni .


Zuchu
Zuchu  binti wa malkia wa mipasho nchini Bi Khadija Kopa, ameibuka hivi karibuni na sauti yake ya tofauti .AnatuImbuza nchi nzima na hit singles zake zote kama, “Nisamehe” , “Wana” zinazozidi kupanda chati kila siku hususan kupitia Kumi za wiki  ameshikilia nfasi ya tatu bora kwa muda mrefu.
 


Nandy
Ni mrembo mtanashati, anaimba na ana kipaji cha kuigiza.   Nandy ama  “The African Princess”, alianza kwa  kuimba kwaya  kanisani,  kwa sasa amaejikita katika muziki wa pop na anafanya vizuri, Nandy pia ni miongoni mwa wachache wenye kipaiji cha kuigiza , anaigiza kaika tamthilia kubwa  nchini ya HUBA , humo kipaji chake kimeonekana kikikua kwa kasi kubwa sana.


Shuhudia taarifa za burudani  , wasanii na mengine mengi Zaidi  bila kusahau simuizi za kusisimua kupitia Maisha magic Bongo DStv160 : BASS kila Jumatatu- Alhamisi saa 11 Jioni, Kumi za wiki kila Ijumaa saa 11 Jioni na Huba kil Jumatatu-Ijumaa saa 3 Usiku.

Images: via Instagram