channel logo dark
channel logo dark

Slay Queen

160Drama16 V

Thamani ya Dada – Huba

Habari
03 Agosti 2020
Jana, tarehe 2 Aogasti ni siku kuu ya madada duniani, tnawapa kipao member madada tofauti ndani ya vipindi vya  Maisha Magic Bongo.
My Post (12)

Wengi wanaweza kukubali kama uhusiano wa mtu na dada yake ni kitu maalum. Dada anaweza kuwa mtu uliyezaliwa nae au mtu ambaye amekuwa karibu na wewe kama familia. Kwenye vipindi vyetu kuna mahusiano tofauti na kila mtu na dada yake, hapa tumechagua madada tunaowapenda.


1. Rani and Ruki: Dhamana la Mapacha (Huba)
Kila mtu anajua kama dhamana la mapacha ni kitu ambacho kina nguvu sana na hakivunjiki kwa urahisi. Penzi kati ya Rani na Ruki ni kali kiasi kwamba baada ya Rani kufariki Ruki aliapa kwamba ni bora yeye achukuliwe kuliko kuona siku njingine bila dada yake kipenzi.


2. Fifi:Dada hodari wa Sudi (Nyavu)
Mahusiano kati ya Sudi na dada yake Fifi yanakuaga na matata mara kwa mara. Lakini Fifi alivyopotea tuliona jinsi Sudi alikuwepo kipao mbele kumtafuta dada yake. Mahusiano yao yanatuonyesha hata kama ukimkasirikia dada yako, mwisho wa siku hamna chochote hautoweza ku fanya kwaajili yake.

 

3. Evelyn: Nguzo ya Derick (Slay Queen)
Derick na Evelyn wamekuwa karibu tangu utotoni, wamekulia kwenye mazingira ambayo sio ya kwaida. Lakini hilo halijawahi kuwafanya wakosane amani. Baada ya kupoteza mama yao na baba yao kuoa Julieth wamejikuta wameback wawili tuu na kila kitu Derrick amejikuta akimtegemea dada yake tuu kwa sababu hana mwanamke mwingine maishani mwake.


Kutokana na haya mahusiano ni dada gani anakukumbusha wewe na mahusiano na dada yako au mwanamke yeyote unamwona kama dada? Usikose vipindi hivi vyote hapa DStv chaneli 160; Nyavu kila Jumatatu mpaka Jumatano saa 1:30 usiku, Huba kila Jumatatu mpaka Ijumaa saa 3:00 na slay Queen kila Jumatano hadi Ijumaa saa 3:30.