channel logo dark
Nyavu Slim BB
channel logo dark

Nyavu

160Drama16

Je Nyavu Imemteka Fifi?

Habari
17 Julai 2020
Mchakamchaka wa msimu wa tatu wa #NyazuTZ unaanza na maswali mengi sana. Lakini swali la muhimu ni “Fifi yupo wapi?”.
Screenshot 2020 07 15 at 11

Tangu Fifi alivyopotea, watu tofauti wameanza kuvutana mashati. Kila mtu karibu nae amebaki akimnyooshea mwenzake vidole. Hili jambo limeishia na mashindano makubwa kuona ni nani kati ya watu wote walio karibu na Fifi atakuwa wakwanza kumrudisha Fifi nyumbani. Kwenye hili shindano, kuna watu wanne ambao wanaongoza kwenye mchakato wa kumleta Fifi nyumbani. Ni vizuri kuangalia kwa karibu mahusiano ya Fifi na watu karibu nae na pia juhudi walizo zifanya kumtafuta Fifi.


1. Sudi
Mdogo wake Fifi, Sudi mwenye hasira na kisasai amekua akitumia hasira na ubabe kumtafuta dada yake. Sudi bado ni mtoto na hajajifunza jinsi mambo ya walimwengu yalivyokua. Ameeanza kukutana na watu wabaya na mara kwa mara anajikuta kijiweni na wahuni. Lakini Sudi anampenda sana dada yake na hakuna kitu hatoweza kumfanya aache kumtafuta dada yake, Damu nzito kuliko maji!


2. Ida
Nani kama mama? Kama kuna mtu ana umizwa na hili ni Ida, mtoto kwa mama hakui na Ida ametuonyesha hili dhahiri! ni vigumu kwake yeye kutofikiria kama amepoteza mwanae kabisa. Ila, kwa jinsi Ida alivyobeba siri nyingi nzito ndani ya ndoa yake ni vigumu kupata msaidizi wa kumtafuta Fifi. Uhusiano kati ya Ida na mwanae unazidi ku didimia lakini pendo la mama haliwezi kutoka.

3. Stoni
Mapenzi  yana nguvu isiyo ya kawaida! yanaweza kumchanganya mtu yeyote, na Stoni sio tofauti. Tangu Fifi kupotea, Stoni amekosa amani sana hata ugomvi na mama yake umezidi mpaka ameamua kumkana mama yake na kumtelekeza mke. Mama yake Stoni ndio bado kikwazo chao sana kwenye mahusiano, lakini mpaka sasa hivi hatujui kama Stoni ataamua kumwacha mke wake awe au laa. 

4. Heri
Heri amegundua hivi karibuni kwamba Fifi ni mwanae, kipao mbele kwake ni kujaribu kuwa na mahusiano na mwanae ili asizidi kupoteza siku bila kuwa kwenye maisha yake tena. Ndoa yake Heri na Lena imefanya Heri azidi kuchanganyikiwa kwenye misheni yake ya kumtafuta Fifi.



Kwa matukio bomba ya kumtafuta Fifi, usikose kuangalia kipindi cha Nyavu kila Jumatatu mpaka Jumatano saa 1:30 usiku, ndani ya Maisha Magic Bongo chaneli 160 pekee.