Tarehe 6 Januari tuliona jinsi mambo yalivyo waka moto ndani ya chaneli bomba nchini Tanzania. Kipindi cha kwanza cha Jua Kali kilianza kuonyeshwa ndani ya Maisha Magic Bongo. Tamthilia hii inahusu bingwa wa hesabu, Profesa Bill, ambaye anatumia watu mbali mbali kufanya uchafu wake. Kipindi hiki kimefanya kazi nzuri ya kuta tamthilia ambayo inaonyesha sekta mbalimbali za jamii na kutupa vitu vingi vya kujadili kama wanajamii pia.
Hapa ni baadhi ya maswala watazamaji wetu wanaendelea kujadili:
1. Mbona huyu professa ana roho mbaya?
Kwa jinsi huyu Professa alivyo mtu hauwezi kufikiria kama anafanya maovu kama hayo, sasa swali linabaki kuulizwa ni nini kilichomfanya awe hivyo?
2. Huyu professa atakuwa na jambo lake ambalo sio bure, inakuaje atoe check harafu mtu akose pumzi?
Kwa ulimwengu ulivyokuwa siku hizi, hamna cha bure. Watu wengi wanauliza ni nini anachofanya ambacho kinamweza kuwa na jehuri hiyo?
3. Mbona mafundi wote wapo #JuaKaliTZ?
Ukiangalia kila kona ya kipindi hii ni mastaa na mabingwa wa kuiza waliojaa kwenye kipindi na pia kuna sura mpya ambazo zinazidi kuonyesha vipaji watanzania walivyokuwa navyo.
4. Mbona wazee wengi wako underground?
Hili ni swali watazamaji wengi walikuwa wakiuliza na labda kwa jinsi tamthilia hii ikiendelea itaweza kusahidia na majibu.
Usikose kuangalia #JuaKaliTZ kila Jumatano hadi Ijumaa saa 3:30 na marudio kila Jumamosi saa 7 mchana ndani ya Maisha Magic Bongo, chaneli 160.
