channel logo dark
channel logo dark

Jua Kali

160Tamthilia16

Bahati mbaya ya Anna – Jua Kali

Habari
11 Agosti 2021
Mapenzi yamemtesa sana Anna
Screenshot 2021 08 11 at 12

Baada ya kukutana na Dr Temba, kili mtu alikuwa amedhani kwamba shida za mapenzi za Anna ndio zimeisha. Lakini, kwa bahati mbaya hayakuishi hivyo. Hii ndio ratiba ya nyakati ya jinsi Anna alivyoteswa na mapenzi:

 

George

Anna alikuwa anafikiria kwamba, yeye na George wataoana baada ya George kurudi Tanzania tokea Marekia. Lakini siku ambayo George alivyokuwa anakuja Tanzania, Anna na familia yake walikuwepo uwanja wa ndege kumpokea nah apo ndipo alipoona kwamba mke wake George na watoto wake walikuwa washamuwahi kumpokea nah apo ndipo alipogundua kwamba muda wote yeye alikuwa ni mchepuko wa George.

 

Dominic

Alivyokutana na Dominic, Anna ndio hivyo alikuwa ameachana na George. Watu wengi walimuonya kwamba kabla ya kuanza mahusiano na Dominic, Anna angejipa muda kidogo. Baada ya mahusiano kidogo, Anna na Dominic waliamua kufunga ndoa na siku ya harusi ndipo Anna alijifunza kwamba rafiki yake wa karibu ndiye aliye mleta Dominic ili amtapeli Anna.

 

Dr Temba

Baada ya mikosi hiyo yote, Anna alikuwa hana hamu tena na mapenzi. Lakini kwa bahati nzuri akakutana na Dr Temba. Dr. Temba alikuwa  mwanaume aliye mpenda Anna kw dhati na kumdhamini mpaka familia yake ikafurahia. Muda sio mrefu ulivyopita waliamua kufunga na kwabahati mbaya kwenye siku ya harusi ajali ilitokea na Dr. Temba akafariki.

 

Baada kifo cha Dr. Temba Anna hajui atafanya nini, usikose kufuatilia #MMBJuaKali kila Jumatano hadi Ijumaa saa 3:30 usiku.