channel logo dark
Season 14
channel logo dark

Huba

160Tamthilia16

Sababu TANO za kuipenda tamthilia ya HUBA!

Habari
06 Juni 2020
Tamthilia hii ni moja ya tamthilia zilizo tamba na kupendwa sana Afrika Mashariki!
Screenshot 2020 06 04 at 10

HUBA inaendela kutoa burudani safi kwa mashabiki wetu. Misukosuko, kasheshe, upambanaji wa mali na mapenzi, bila kusahau elimu kwa jamii ni baadhi tu  matukio yanayoleta mbwembwe ndani ya HUBA. Je ni nini haswa kinachowavutia watazamji wetu kwa wingi?  Hizi ni sababu kuu tano kwa nini tunaipenda tamthilia ya HUBA:

 

1.  Mapenzi, huba na mahaba yanaweza kujenga au kubomoa:

Safari ya Tima na Devi kuanzia mwanzo penzi la moto kati ya tajiri na maskini. Heka heka walizopitia enzi za Batuli na Kibibi, na sasa Rani, ni ngumu kuamini penzi lao lingebaki kuwa imara. Chidi naye kujiopolea Kibibi na kutelekezwa badaaye. Mzee Kashaulo na wake zake BI Mgeni na Sidi pamoja na Upambanaji wa Doris kuhakikisha Roy anabaki kuwa wake. Tesa kamua kugeukia mapenzi ya ben ten, japo ana njama na mipango chungu nzima, bado moyo wake unapata pakupumzikia usiku! Je Chidi na happy watatupa makopa kopa nao au itabaki stori? Kwa kifupi mapenzi yanatawala daima.

 

2. Adui ya adui wangu, ni rafiki yangu:

Tamaa mbaya! Sidi alihifadhiwa kwa Tima muda mrefu tu akiwa hana makazi hana mbele hana nyuma, kuingia tu humo ndani kamuibia shosti yake Bi Mgeni mume na kaungana na Tesa kubwa la maadaui kumtokomeza Tima kisa tu viahadi alivyopewa na Tesa, kusema ukweli alibadilishiwa maisha kwa muda nyumba nzuri maisha ya uswazi tena basi visenti vya hapa na pale na mengine mengi , bila ya yeye kujua alijikuta anajiingiza katika vita visivyo vyake! Kuiba vyeti vya Fuli Jr kumpelekea Tesa yanamtokea puani !! kweli kabisa Mwana kulitafuta mwana kulipata , sio tu huba lake lipo hatarini hata Tesa mwenyewe kamkana.

 

3. Tunasimama imara – Tima ,Devi , Roy na Nandy!

Mahusiano kati ya Devi na Tima hayajawahi kuwa mepesi, haswa kwa upande wa Tima. Devi amempelekesha mbio sana , maskini Tima. Nandy na Roy penzi lao limesimama imara mpaka hatua za kufunga ndoa lakini, penzi la zamani lina poromosha kila Kitu Bi dada Doris kafanikiwa kuvuruga kila kitu je ndoa yao itawahi kufungwa tena ?  na Tima mjamzito tena mtoto wa pili wa Devi , je Tesa atafanya nini?

 

4. Mapenzi Pesa Bwana!

Jude, kaka wa mjini chipukizi, mpenda-nakshi na pesa mbele siku zote, anajitegesha na kumteka Ruki kimapenzi, akidhania ataokota dodo kumbe dodo limeoza. Pesa alizodhania Ruki anazo, hana bali, ni za Rani na Devi.  Mzee baba katoka kapa kabisa na kuamua kujisepea, kamuacha mkwewe kwenye mataa. Mwingine ni Tesa na Pedro. Je ni mapenzi ya dhati au ni kutumiana tu.

 

5. Changu ni chako:

Kibibi anateuliwa katika biashara haramu ya Mzee Ngote. Maisha ya Kibibi yamebadilika mazima,  kaangukia kwenye penzi la mzee tajiri jijini Zanzibar  alipokimbilia akimkimbia aliyekuwa mume wake Chidi.  Huko, anakutana na mengi, lakini, la msingi kwa sasa yeye ni mke halali wa tajiri Ngote.  Je, mwanae Ngote atakubali?

Ungana nasi kila Jumatatu hadi Ijumaa saa 3 usiku kupiita chaneli bingwa katika simulizi zetu za kinyumbani! Tazama highlghts hapa!