channel logo dark
Season 14
channel logo dark

Huba

160Tamthilia16

Njama za mapenzi - Huba

Habari
27 Aprili 2020
Wachumba na wanandoa wa HUBA kwa pamoja, wamelipa swala  ‘’MAPENZI’’ maana mpya kabisa! Swala la leo, watu wako tayari kufanya nini kutekeleza malengo yao katika maisha ya ndoa na mapenzi?
<p>HUBA article cover</p>

 Jude ameamua kuwaomba wazazi wa Ruki ruhusa ya kufunga ndoa. Roy na Nandi penzi lao linaonekana kustawi kila siku na kazi zao pia, zinaendela vizuri.

Kwa upande mwingine Bi dada Kibibi na Mzee Ngote, mmh? Je, huu ni mwanzo wa huba au kuna nini kati yao? Wawili hawa, bado wanatuacha na maswali mengi!

Kiukweli, wana huba kila kukicha, wanatuacha na maswali mengi sana.

 

Dave , Rani na Tima! Mtihani aliyo nao Dave katika mapenzi ni mkubwa sana, huku mama wa mtoto wake Tima  na Rani pia. Alianzisha mahusiano na Rani kipindi alipopoteza fahamu, akiwa Idris. Sasa, fahamu zimerudi na mapenzi yanonekana kuegemea upande wa mama mtoto wake Tima. Rani naye, hakubali kushindwa!

Je, ni nani anatamani kuva viatu vya Dave?

 

Tesa, ambaye daima anaonekana kuwa na mahusiano na 'vi ben ten' na asiyependa kabisa mahusiano ya mwanaye wa pekee Dave na Tima, safari hii, kaungana na Bi sikitu kuhakikisha mipango yake yote inakaa sawa.

Kibibi na Ngote! Wawili hawa walikutana katika mazingira tusiyo yategemea kabisa na kutoka kuwa bosi wake na sasa hivi mzee wetu anaonekana kukolea katika huba la Bi Kibibi . Je Kibibi ata ridhia kuwa mke wa Mzee Ngote?

Wenye mapenzi ya kudumu kabisa Mzee Kashaulo na Sidi ambao ni wanandoa wa miaka mingi. Safari yao haikuwa rahisi lakini wawili hawa wanaonekana kudumu na kutoka utajiri umaskini jua na hata mvua.

WIKI HII!

Kibibi  Kafunguka kwa Ngote yote kuhusu Maisha yake , Dave katangaza rasmi kuwa sasa anatumia jina la Dave, Tesa  anasherehekea na bado hataki kabisa kumsikia Tima,  Ruki  alianza safari ya mapenzi na Jude kwa nia tofauti kabisa na sasa anaokeana kama anazama kikweli kweli kabisa, mipango ya harusi imeaanza,  Rani analizwa na Dave je atafanya maamuzi gani?. Pata highlights za wiki hii hapa na usibanduke! Chaneli ni DSTv  160, Maisha Magic Bongo! Ni yetu!

Fuatilia HUBA kila Jumatatu hadi Ijumaa saa 3 usiku ndani ya MMBongo pekee!