channel logo dark
Season 14
channel logo dark

Huba

160Tamthilia16

Kibibi apata kazi — Huba

Habari
15 Machi 2020
Je atafaulu kufanya kazi na kumlinda mtoto?
huba, tanzania soapie, tamthilia ya huba

Kibibi amepata kazi hotelini lakini anakuwa na wakati mgumu kwa ajili ya mtoto wake. Meneja wa hoteli hajafurahi na yeye kwa sababu mtoto wake anashinda akilia. Je ataendelea na kazi ama ataamua kuwacha kazi ili amlee mtoto wake?

Ruki na Rani bado wanamandama Doris ambaye ameandikwa kazi na Davy. Ruki anaudhika pale Tima nanaletea Davy chakula cha mchana. Doris anaamua kumpa Rani mawaidha na kumshauri kwamba ni muhimu awe na subira, ujanja na mpole wakati anapohusiana na Davy. 

Kwingine baada ya Mgeni kutimuliwa na Tima nyumbani mwake, Kashauro anaanza kuwa na wasisi akitaka kujua ako wapi. Jambo ambalo hajui ni kwamba ametekwa nyara na Bi Sikitu, kama alivyoamrishwa na Sidi.

Roy anafaulu kumuandalia mpezi wake Nandi sherehe ya kufana sana na Tesa na Pedro wanaendelea kuwa na uhusiano wa karibu. Carlos anaendelea kuiba chakula kutoka kwa Sidi na Stano anaamua kulea mtoto wake mwenyewe. 

Tazama highlights zaidi hapa

Fuatilia Huba kila Jumatatu hadi Ijumaa saa 3 usiku.